Mwandishi wa habari Mmisri Amira Sayed anashiriki katika mpango wa mafunzo juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na usalama wa maji nchini Ethiopia

Taasisi ya Kimataifa kwa maji huko Stockholm inachagua mwandishi wa habari Mmisri Amira Sayed, Raisi wa Bunge la Misri kwa maji kwa kuhudhuria programu ya mafunzo juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na usalama wa maji nchini Ethiopia,
Na hiyo kwa ushiriki wa waandishi wa habari kadhaa kutoka Misri, Ethiopia, Sudan na Sudan Kusini.Programu hii ya mafunzo imeandaliwa kwa kushirikiana na shirika la  UNESCO kwa Elimu, Sayansi na Utamaduni.

Inatajwa kuwamba Amira hivi karibuni alishiriki katika hafla kadhaa, hasa ushiriki wake wa hivi karibuni katika mkutano wa kilele cha Afrika huko Niger chini ya malengo ya Umoja wa Afrika na alipata jina la balozi mchanga wa Amani , Mmisri wa kwanza kupata jina hili.
Amira pia alishiriki kama msemaji katika shughuli za wiki ya kiarabu ya maendeleo endelevu inayodhaminiwa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu
katika kikao kilichoitwa "Jukumu la wanasayansi wachanga katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu" .Na alisisitiza jukumu la uandishi wa habari katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu.

Comments