Waziri wa Michezo anashuhudia shughuli za mkutano wa Kimataifa kupambana na ufisadi wa kimichezo Barani Afrika
- 2019-12-07 18:39:30
Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa Vijana na Michezo, na Jenerali Ahmed Nasser Rais wa Shirikisho la Muungano wa kiafrika "Auxa", na Dokta Mustafa Baraf Rais wa Jumuiya ya Kamati za Olimpiki ya kiafrika, walishuhudia kuanza kwa shughuli za Mkutano wa Kimataifa kupambana na ufisadi wa kimichezo barani Afrika,ambao shughuli zake zitadumisha hadi Desemba hii 8 chini ya uangalifu wa Rais wa Jamhuri Mheshemiwa Rais Abdel Fattah El Sisi.
Mkutano huo ulishughulika katika maswala kadhaa kwenye uwanja wa kupambana na sura za ufisadi katika taasisi za michezo barani Afrika, na athari mbaya ya vyombo vya habari na maoni ya umma katika kuunga mkono uzushi wa ufisadi wa kimichezo na jukumu la jamii katika kupambana nayo,na kuanzisha kanuni na njia za kupigania, wanawake na michezo katika mfumo wa kupambana na ufisadi katika michezo, na kikao cha kufunga kwa mkutano huo utafanyika ambao mapendekezo yataonesha kuwasilisha kwa serikali , mashirikisho ya kimichezo katika nchi za kiafrika.
Waziri wa Vijana na Michezo Ashraf Sobhy alisisitiza kuwa serikali ya Misri itafuata kwa hamu matokeo ya mkutano huo wa kimataifa wa kupambana na ufisadi wa kimichezo barani Afrika, na aliongeza kuwa wizara hiyo inatafuta kufikia hatua muhimu zinazochangia kukomesha ufisadi wa kimichezo na kuweka maoni mbele ya viongozi ili kupambana na ufisadi wa kimichezo na michakato ya kuukabili, akiashiria kwa msaada wa wizara kwa mkutano huo na uangalifu wa mafanikio yake na kufanikisha malengo yake yanayotaka.
Sobhy aliashiria kwamba michezo ya Kiafrika ilifanikisha maendeleo ya haraka na ya kuvutia katika kipindi cha mwisho.
Waziri huyo alimalizia kwa kusema kwamba anafurahi kuwa mkutano huo utafuatana na shughuli nyingi zinazofanana, ikiwa ni pamoja na kuanzia na kutangazwa kwa tuzo ya ubora wa michezo kwa kikundi cha alama za michezo za Kiafrika, katika mahudhurio ya idadi ya wahusika wakuu kutoka nchi tofauti.
Kwa upande wake , Jenerali Ahmed Nasser alisisitiza kwamba lengo la mkutano wa kwanza wa kimataifa wa kupambana na ufisadi wa kimichezo barani Afrika ni kuondoa ufisadi kwa njia kamili ndani ya mashirikisho ya mabara .
Sherehe ya ufunguzi ilihudhuriwa na Jenerali Mohamed Nour Mkurugenzi Mtendaji wa Wizara ya Vijana na Michezo, Dokta Emad Al-Bennani Katibu Mkuu wa Shirikisho la muungano wa kiafrika, Dokta Ahmed Sheikh kaimu wa wizara kwa mambo ya Ofisi ya Waziri, baadhi ya mabalozi wa Kiafrika walioshiriki katika mkutano huo, baadhi ya wakuu wa mashirika ya kiafrika na kikundi cha wahusika wakuu na kimichezo.
Hafla ya ufunguzi ilishuhudia tamasha la muziki lililotoa na Orchestra "Bendi" ya Wizara ya Vijana na Michezo.
Comments