kocha wa timu ya kitaifa ya Sarakasi ya Urusi amefika mjini Kairo ili kuanza uteuzi wa wachezaji wa timu ya kitaifa ya Sarakasi ya Kimisri ya wanawake kwa ajili ya uandaaji ili kushiriki katika michuano ya Kiafrika itakayofikia kikao cha michezo ya Olimpiki Tokyo 2020, baada ya shirikisho la Sarakasi chini ya uongozi wa Dokta Ehab Amin limesaini mkataba rasmi pamoja na kocha huyo.
Kocha alifuatana naye timu ya kitaifa ya sarakasi ya Urusi ili kuingia katika kambi iliyofungwa mjini Kairo kwa muda wa mwezi mmoja mpaka wakati wa mwisho wa mkataba wake rasmi na shirikisho la Urusi, 9 Januari 2020.
Iliyopangwa kuwa kocha wa Urusi atateuzi wachezaji wa timu ya kitaifa ya Sarakasi ya Kimisri kupitia mitihani ya kiufundi kwa wachezaji wa klabu zote, mnamo kipindi cha tarehe 9 Desemba mpaka siku ya 9 Januari, mwaka ujao.
Ehab Amin, mwenyekiti wa shirikisho la Sarakasi aliyeweza kusaini mkataba na kocha wa Urusi baada ya majadiliano yanayoendelea kwa muda mrefu, amesisitiza kuwa kuna viwango vikali vya kiufundi vilivyowekwa na kocha wa Urusi mbali na pongezi katika uteuzi wa wachezaji wa timu ya kitaifa ya Misri.
Pia aliongeza kusema kwamba kocha huyo wa Urusi ni nyongeza kubwa kwa Sarakasi nchini Misri kwa ajili ya kuendelea katika mabadiliko ambayo shirikisho linayafanya.
Amin aliashiria kuwa uwepo wa timu ya kitaifa ya Sarakasi ya Urusi katika kambi iliyofungwa kwa muda wa mwezi mmoja mjini Kairo na kufanya mazoezi pamoja na timu ya kitaifa ya Misri chini ya uongozi wa kocha mmoja utazidi wachezaji wa Misri kwa ujuzi wa kimataifa ambayo timu ya kitaifa ya Urusi inazimiliki.
Shirikisho la Sarakasi la Kimisri chini ya uongozi wa Ehab Amin limekuwa kusaini mkataba pamoja na kocha wa timu ya kitaifa ya Urusi na aliyeainishwa kama kocha wa kwanza ili kuundwa kwa timu ya kitaifa ya Sarakasi ya Kimisri, kwa matamanio ya kufikia Tokyo 2020 na kizazi kikali Mwenyezi Mungu kipenda.
Comments