Uteuzi wa miji miwili ya Kairo na Hurghada miongoni mwa miji ya kitalii 100 bora zaidi ulimwenguni

Miji miwili ya Kairo na Hurghada iliteuliwa miongoni mwa miji ya kitalii 100 bora zaidi ulimwenguni, hii kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na taasisi ya ( Euromonitor international) inayo utaalamu katika masoko, ambapo utafiti umekamilika kwenye zaidi ya miji 400 ulimwenguni kwa msingi wa idadi za watalii wanaokuja mnamo mwaka wa 2018.

Ripoti ilionyesha kuwa miji ya kitalii 100 iliyoiteuliwa inatofautisha na ukuu wao unaoendelea katika ongezeko la idadi za watalii wanaokuja kutoka nchi za dunia, ambapo utalii utakuwa kichocheo cha uvumbuzi pamoja na kuwa miji hiyo ni injini ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi, pia ripoti hiyo imeashiria kuwa miji inazingatia lango la uchumi, ambapo mabadiliko ya miji yanayoendelea inafanya kubadilisha katika njia ya watalii pamoja na miji na jaribio lake na pia aina ya watalii ambao wanawavutiwa mjini.


Dokta Rania Almashat Waziri wa utalii amepongeza Misri, akiashiria kuwa iliyotolewa na ripoti hiyo inakuja miongoni mwa mfululizo wa kimataifa wa kusifu ambayo utalii wa Kimisri umeupatia, na akisisitiza kuwa jambo hilo linaonesha mwonekano wa ulimwengu kwa Utalii wa Kimsri kwa utekelezaji wa mpango wa mabadiliko ya miundo ili kukuza sekta ya utalii ambayo inazingatia nguzo ya msingi ili kuhakikisha mafanikio na kukua kwa sekta hiyo.

Comments