"Wizara ya vijana na Michezo " inapanga Kampeni kubwa zaidi ya kujitolea ya kiafrika ili kuyasafisha maji ya Nili na kuilima miti mia moja kwenye eneo la 15 Mei

Wizara ya Vijana na Michezo "Idara kuu kwa Bunge na Elimu ya kiraia na ofisi ya Vijana waafrika " na Kameshina ya Umoja wa kiafrika, zilipanga tukio kubwa zaidi la kujitolea la Vijana waafrika, lililokusanya kampeni ya kuyasafisha mto wa Nili pamoja na Kashafa "Kundi "la bahari, kwa kushirikiana na wanajitolea Waafrika 200 na hiyo kwa ushirikiano na Wizara ya Umwagiliaji na taasisi ya vijana wanaipenda Misri.

Pia wanajitolea wa Umoja wa kiafrika walilima miti 100 kwenye eneo la 15 Mei, na hayo yalitokea wakati wa matukio ya siku ya nane kutoka programu ya wanaojitolea wa Umoja wa kiafrika kwa toleo lake la kumi, chini ya usimamizi wa Mheshemiwa Rais Abd Elfatah Elsisi.


Na inatajwa kwamba programu ya wanaojitolea wa wa Umoja wa kiafrika(AU-YVC) ni Programu kubwa zaidi ya kujitolea inayoteklezwa kwa Umoja wa kiafrika barani Afrika; ambapo tukio hilo linakusanya vijana wanajitolea kutoka nchi tofauti za kiafrika, na mwaka huu hupokewa kwa Kairo huko kituo cha Kiolimpiki, mnamo kipindi cha Desemba 1-12 mwaka huu, na kundi la kumi linakusanya Vijana na wasichana waafrika 200 toka nchi 54 za kiafrika;kwa hiyo inazingatiwa tukio la kwanza la kipekee pia katika historia ya kulipokea tangu utoaji wa toleo lake la kwanza mwaka wa 2010.

Comments