Mawaziri wa Vijana na wa Mabaki ya kale wanakutana na washiriki wa mpango wa kujitolea wa umoja wa kiafrika
- 2019-12-11 13:04:11
Dokta Ashraf Sobhy waziri wa vijana na michezo alikutana na waziri wa Mabaki ya kale Dokta Khaled Al anani pamoja na vijana wanaoshiriki katika mpango wa kujitolea wa umoja wa kiafrika iliyofungwa chini ya udhamini wa Rais Abdel Fatah El sisi mnamo kipindi cha 1-12 Desemba katika kituo cha olimpiki huko Maadi imeandaliwa na wizara ya vijana na michezo kupitia ( idara kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia - ofisi ya vijana waafrika ) na kameshina ya umoja wa kiafrika
mfano wa kuiga unakuja katika mfumo wa kuwawezesha vijana wa kiume na wa kike barani Afrika kujitolea kwa miezi 12 ndani ya umoja wa kiafrika , programu ya kujitolea ya Au ( Au - YVC) ndio mpango mkubwa zaidi wa kujitolea barani Afrika , ilianzishwa mnamo 2010 inafanya kazi kupatana na Ajenda ya umoja wa kiafrika 2063 , inakusudia kuwezesha makada wa vijana kufanya kazi kwenye ajira zao katika nyanja za maendeleo ili kutumika nchi zote za kiafrika katika sekta tofauti.
katika hotuba yake , Dokta Ashraf Sobhy alisema : ni chanzo cha kujivunia na kufuruhisha kwamba wizara ya vijana na michezo inawakaribisha vijana wa afrika kukutana pamoja katika seti ya mipango na miradi ya kubadilishana tamaduni kati yao kufikiria juu ya siku zijazo za kiafrika kuelekea kazi zaidi , ujenzi , maendeleo, umoja na ujumuishaji wa juhudi
waziri wa vijana na michezo alikaribisha kwa kuhudhuria waziri wa Mabaki ya kale kwa mpango ya kujitolea ya Au na semina juu ya uvumbuzi na maendeleo yaliyoshuhudiwa katika faili ya akiolojia ya Misri
kwa upande wake , waziri wa Mabaki ya kale alitoa muhtasari wa historia ya zamani ya Misri pamoja na uwasilishaji uliojumuisha seti ya video kwenye uvumbuzi wa akiolojia wa hivi karibuni ili kuanzisha vijana wa kiafrika kwa ustaarabu wa Misri na makaburi yake ya zamani
waziri pia aliwasilisha juhudi za Misri zilizowekwa katika uratibu na ushirikiano uliopo na nchi kadhaa katika kurejesha mabaki ya kuingizwa , kwa kuongeza juhudi za wizara ya Mabaki ya kale katika utekelezaji wa miradi ya kumbukumbu na utunzaji na marejesho na ukuzaji wa tovuti za akiolojia katika mikoa mbalimbali
Comments