Dokta Ashraf Sobhy anayafungua majengo kadhaa kwa vijana na michezo kwenye mikoa tofauti ya Jamhuri

Mnamo siku chache zijazo, Dokta Ashraf Sobhy "waziri wa Vijana na michezo "anayafungua majengo kadhaa kwa vijana na michezo kwenye jamhuri, ambapo ufunguzi huo unavijumuisha vituo kadhaa vya vijana, na baadhi ya majengo ya kimichezo ndani ya klabu baada ya kuyaboresha,na kuongeza ufanisi wake kwa njia inayofaa jicho la taifa kwa jambo hilo.

 

Na katika jambo hilo, waziri wa vijana na michezo amesisitiza kwamba uongozi wa kisiasa umeonyesha dharura ya kuyaangalia na kuyaendeleza majengo yote ya vijana na michezo, kwa njia inayowafikiana na mahitaji ya mtu khasa katika vijiji na mitaa, pia mikoa yenye mipaka, akiashiria kwamba katika kiwango cha kwanza taifa linaangalia na kutosheleza mahitaji yote ya mtu na jamii ambayo yenye umuhimu zaidi ni mahali pa kucheza michezo, na pia kujenga miradi yenye malengo ya kutoa ubunifu wa vijana na wenye ulemavu na shauku.

 

Na Dokta Ashraf Sobhy ameongeza kwamba wizara ya vijana na michezo inatoa mchango muhimu wa kuhakikisha maendeleo endelevu ya kijamii, na kutosheleza idadi ya miradi, Programu, na harakati zinazolenga kwa jambo lile, akionyesha kwamba mnamo awamu ijayo, mpango wa wizara uliboreshwa kwa njia inayofaa kwa mtazamo wa taifa 2030.

 

Na hayo yote yanakuja kulingana na mkakati wa kujenga mwanadamu wa kimisri uliotoa mkakati wa wizara ya vijana na michezo unaozingatia pande za kitaaluma, kimwili, kijamii, na kiuchumi kwa makundi yote ya jamii.

 

Na inayohusishwa pia hapa ni kwamba wizara ya vijana na michezo inachangia kutekleza idadi ya hakati na Programu za kimichezo kwenye miradi mikubwa ya kitaifa na kimaendeleo kama " Mlima wa enzi", "Mji mkuu mpya wa kuongoza" na menginyo yanayoangaliwa kwa taifa pia yanayosaidiana kufungua njia mpya za kiuwekezaji, kiuchumi,  zenye lengo la maendeleo na kuunga mkono kwa ngazi zote, ili kuzitambulisha kwa vijana na ukubwa wa mafanikio yaliyofanywa kwa serikali, kupitia kujenga miradi mikubwa ya kitaifa ambayo daima ina athari adhimu ya kuhakikisha maendeleo endelevu kwa ngazi zake zote.

Comments