Barua ya shukrani kutoka CAF kwa uandaaji wa kombe la mataifa ya Kiafrika chini ya miaka 23

Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi wa shirikisho la Soka  la Kimisri na mwenyekiti wa kamati iandaayo michuano ya kombe la mataifa ya Kiafrika  Amr Alganyny ameipokea barua ya shukrani kutoka shirikisho la soka la Kiafrika kwa uzuri wa uandaaji wa michuano iliyoelezwa na CAF kuwa michuano isiyo kusahaulika, pia katika barua hiyo kuna salaamu kwa mamlaka inayohusika juu ya ushiriki katika uandaaji huo wa kipekee.... Na maandishi ya barua yalikuja kama ifuatavyo :


Bwana / Amr Alganyny

Mwenyekiti wa Kamati iandaayo michuano ya kombe la mataifa ya Kiafrika chini ya miaka 23 - Misri 2019

Mpendwa wangu bwana Alganyny,

Kwanza, tunapenda kukupongeza kwa mafanikio ya kipekee ya kombe la mataifa ya Kiafrika chini ya miaka 23, Misri 2019, na ushindi wa timu ya kitaifa ya Misri ya Olimpiki na kufikia kwake Olimpiki Tokyo 2020.

Pili, tunataka kukushukuru kwa uandaaji wa kipekee wa kombe la mataifa ya Kiafrika chini ya miaka 23, Misri 2019, na hali nzuri zilizotolewa kwa shirikisho la soka la Kiafrika na timu za kitaifa zote zilizoshiriki katika michuano hiyo.

Ushiriki wa serikali ya Kimisri na juhudi za wanachama wa kamati iliyoandaa michuano hiyo umekuwa sababu ya kufanikiwa kwa tukio la kihistoria hilo, kwa hivyo, tafadhali toa shukrani zetu kwa mamlaka za Kimisri na wanachama wote wa kamati iliyoandaa michuano hiyo.



Kamati inayoandaa michuano hiyo ilitoa shukurani zake kwa taasisi zote za nchi zilizoshiriki katika uandaaji huo, pia ilitoa shukurani maalumu kwa mhandisi Hosam Alzanaty ambaye ni mkurugenzi wa michuano hiyo na ambaye ni mkurugenzi mdogo zaidi wa michuano ya bara katika umri na amehakikisha mafanikio makubwa.


Comments