Kwa Naiba ya mkuu wa Kameshina ya Umoja wa kiafrika, programu ya wanajitolea kwa Umoja wa kiafrika inampokea mjumbe wa Umoja wa kiafrika kwa vijana
- 2019-12-11 13:18:39
Wakati wa matukio ya Programu ya wanaojitolea wa Umoja wa kiafrika, inayofanyika chini ya usimamizi wa Mheshemiwa Rais Abd Elfatah Elsisi, Rais wa Jamhuri, na inayopangwa kwa Wizara ya Vijana na Michezo, programu imempokea mjumbe wa Umoja wa kiafrika Bibi Aya ElShabi kama naibu kwa mkuu wa Kameshina ya Umoja wa kiafrika, na hayo miongoni mwa vikao vya majadiliano vya programu.
Na programu ya wanaojitolea wa Umoja wa kiafrika hufanyika kwenye kituo cha Kiolimpiki huko ElMaadi mnamo kipindi cha Desemba 1-12 mwaka huu ili kuwawezesha vijana na wasichana pembezoni mwa bara la Afrika ili kujitolea kwa miezi 12 ndani ya vyombo vya Umoja wa kiafrika.
Na kikao hicho kilizunguka kuainisha Aya Elshabi mjumbe wa vijana waafrika kwa miaka miwili ili kuwa msichana wa kwanza toka kaskazini mwa Afrika kupata nafasi hiyo, na jukumu lake kwenye suala hilo, pia Bibi ElShabi alizungumzia umuhimu wa programu ya wanaojitolea wa Umoja wa kiafrika kama chombo kikuu cha kuwawezesha ndani ya Umoja wa kiafrika.
Pia kikao kilihusisha na jukumu la vijana kwa jamii zao, mchango wao katika Maendeleo ndani ya nchi zao katika nyanja tofauti, na mipango ya vijana inayosababisha Maendeleo na ustawi wa jamii.
Inatajwa kwamba programu ya wanaojitolea wa Umoja wa kiafrika (AU-YVC) inazingatiwa programu kubwa zaidi ya kujitolea barani Afrika, ilizinduliwa mwaka wa 2010 na hufanya kazi sambamba na Ajenda ya Umoja wa kiafrika 2063, na inalenga kuwawezesha vijana ili kupata ajira kwenye nyanja za kimaendeleo katika nchi tofauti za kiafrika katika sekta na taasisi tofauti.
Comments