Waziri wa anga ya kiraia anaangalia uwanja wa ndege wa Sharm ElShekh kabla ya uzinduzi wa mkutano wa vijana wa kimataifa
- 2019-12-13 13:31:59
Mnamo siku ya Alhamisi terehe ya 12/12/2019 Jenerali Younis El Masri ambaye ni, waziri wa anga ya kiraia aliangalia uwanja wa ndege wa mji wa Sharm El-Sheikh ili kuhakikisha maandalizi ya mwisho ili kuwpokea wajumbe wanaoshiriki katika mkutano wa vijana duniani wa mwaka 2019 utakaofanyika mjini Sharm El-Sheikh mnamo kipindi cha mwezi huu kati ya siku 14 na 17 .
Na waziri wa Anga ameshafanya mzunguko wa kuangalia kwenye kumbi za kusafiri na kufika kwenye uwanja wa ndege ,na pia aliangalia hatua zote za usalama ndani na nje ya uwanja wa ndege pia uzio wa nje na kamera za uchunguzi. Pia aliangalia uwanja wa ndege . Na alihakikisha huduma zinazotolewa kwa wasafiri na pia kaunta zilizoteuliwa kwa kukamilisha taratibu za kusafiri na kufika. Pia waziri alizisifu juhudi zilizofanyika kwenye uwanja wa ndege ili kuonyesha uwanja wa ndege vizuri kwa wageni .
Na aliomba kutoa huduma zote kwa wageni wa Misri wanaoshiriki kwenye tukio hilo kubwa linalopokea vijana kutoka nchi mbalimbali duniani walio na athari kubwa katika jamii zao.
Alisisitizia kuwa wafanyikazi wote katika viwanja vya ndege vya kimisri wana jukumu na ujasiri wa kuonekana heshima mbele ya wageni wa Misri kutoka nchi mbalimbali za dunia wakati wa matukio muhimu ya kimatifa yanayofanyika hapa nchini Misri .
Na pia Mwanahewa Wael El-Nashar amabye ni mwenyekiti wa shirika la kimisri la viwanja na pia Mwanahewa Sadik El-Shury ambaye ni mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa kimatiafa wa Sharm El-Sheikh walimfuatana na waziri wa anga.
Na kwa upande mwengine , uwanja wa ndege wa Kairo uliandaliwa kwa kupokea wajumbe wanaoshiriki katika mkutano kupitia kuweka mibango inayohusiana tukio hilo ndani kumbi za kusafiri na kufika na pia kuunda kundi la mahusiano ya kijumla na pia kuandaa kaunta ili kukamilisha taratibu za kusafiri kwa wageni ili kufika mji wa Sharm El-Sheikh kwa njia rahisi sana .
Comments