Taasisi ya ndoto ya kiafrika 2063 ilipanga safari ya bure kwa idadi kadhaa za watoto wa jamii za kiafrika waliopo nchini Misri kwa viwanja vya Dream Park katika eneo la sita Oktober
Na zaidi ya watoto waafrika 50 walishiriki katika safari wakiongozwa na wenzao kuelekea viwanja vya Dream Park kutoka jamii ya Sudan Kusini , Sudan , Chad , Niger na jamii nyingine na hivyo ni katika mfumo wa shughuli ya taasisi ya ndoto ya kiafrika ili kuzisaidia jamii za kiafrika Nchini Misri
Na Sally Atef mkuu wa taasisi ya ndoto ya kiafrika 2063 alisema kwamba taasisi inafanya juhudi ili kuzisaidia jamii za kiafrika zilizopo nchini Misri kupitia shughuli za burudani , kijamii , kimatibabu na kitamaduni mbalimbali . Akielezea kwamba safari hiyo ni miongoni mwa shughuli hizo ambazo taasisi ilizianza kupitia Mikutano ya matibabu kwa kushirikiana na hospitali na madaktari katika utaalamu mbalimbali
Na Sally Atef alisisitiza kwamba jamii za kiafrika nchini Misri wanahitaji sasa huduma hizo za kijamii , akielezea kwamba taasisi ataweka katika mpango wake wa siku zijazo upanuzi wa shughuli zake ili kuzihudumia idadi kubwa zaidi za jamii tofauti za kiafrika nchini Misri kwa kushirikiana na pande nyingi zinazosaidia taasisi na juu yao mwanamke anayefanya biashara Rawya Mansour Mhusika mwenye ushawishi mkubwa barani Afrika katika mwaka huu
Na taasisi ya ndoto ya kiafrika ilizizindua kupitia kipindi kilichopita huduma nyingi kwa jamii za kiafrika na kichwani mwake mikutano ya matibabu kwa kushirikiana na hospitali ya watu binafsi na idadi kadha za balozi za kiafrika nchini Misri pamoja na uzinduzi wa kongamano la uwekezaji wa kimsri-kiafrika ili kusaidia uwekezaji wa pamoja kati ya Misri na nchi za kiafrika
Comments