Timu ya kitaifa ya Misri ya kayaki na kipera imeshinda michuano ya kiarabu ya kumi 2019 na iliyofanyika katika mji wa (Alalamen Aljadida).
Misri imehakikisha nafasi ya kwanza kwa pointi 171, ambapo timu ya kitaifa imehakikisha medali saba za kidhahabu, medali nane za kifedha na medali tatu za kishaba.
Timu ya kitaifa ya Algeria imekuja katika nafasi ya pili kwa pointi 158, ambapo imeshinda medali 5 za kidhahabu, medali 7 za kifedha na medali 5 za kishaba.
Pia katika nafasi ya tatu imekuja timu ya kitaifa ya Iraq kwa pointi 83, ambapo imeshinda medali 5 za kidhahabu, medali mbili za kifedha na medali moja ya shaba.
Timu ya kitaifa ya Morocco imechukua nafasi ya nne kwa pointi 41, kisha timu ya kitaifa Tunisia katika nafasi ya tano kwa pointi 17, pamoja na timu ya kitaifa ya Kuwait katika nafasi ya sita kwa pointi 12, kisha Palestina katika nafasi ya saba na Saudi Arabia katika nafasi ya nane.
Comments