Ashraf Subhi akutana na Mawaziri wa vijana wa Nigeria, Gambia, Chad na Sierra Leone huko Aswan

Dkt .Ashraf Subhi Waziri wa Vijana na Michezo , Raisi wa Ofisi ya Mtendaji wa baraza la Mawaziri wa Vijana wa Kiarabu alikutana na Juffumin Jakob, Waziri wa Vijana wa Nigeria, Mohamed Nasrallah Abdullah, Waziri wa Vijana nchini Chad , Mohamed Bangora, Waziri wa Vijana wa Sierra Leone ,  Waziri wa Vijana na Michezo ya Gambia, Drami Sidi Bey na Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Vijana na Michezo nchini Palestina .

Hii ilikuja kwa upande wa Jukwaa la Vijana wa kiarabu na  Kiafrika  lililofanyika mjini Aswan katika kipendi kutoka 16 hadi 18 Machi ,2018 Chini ya ulinzi na uwepo wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Misri.

Dkt. Ashraf Subhi alikubaliana na Mawaziri wa Vijana na Michezo wa kiafrika wakati wa mkutano, ili kuanzisha mahusiano kati ya nchi mbili, kubadilishana uzoefu kwenye sekta ya vijana na michezo, kutekeleza mipango ya pamoja na ziara, na kuingiza misingi ya ushirikiano wa pamoja katika protokali ya pamoja itakayosainiwa na kila nchi,baada ya uratibu na mamlaka husika wakati ujao. Waziri wa Vijana na Michezo pia alifafanua mfululizo wa mipango mbalimbali itakayofanywa na Wizara mwaka huu na kwa kushirikina wizara za vijana wa nchi za Kiafrika katika shughuli za "Aswan, mji mkuu wa vijana wa Afrika", uliotangazwa na  Raisi Abdel Fattah El-Sisi,na Dkt Subhi amewaita vijana wa bara kwa  kushiriki katika matukio haya.

Kwa upande wao, Mawaziri wa Vijana na Michezo walisifu wazo la kuanzisha Jukwaa la Vijana wa kiarabu na  Kiafrika chini ya ulinzi  wa Raisi Abdel Fattah El-Sisi  Raisi wa Misri na Rasi wa Umoja wa Afrika 2019 .

Comments