Mhandisi Ahmed Mujahid, Mratibu Mkuu wa Kombe
la Mataifa la Afrika 2019 ,alisema kwamba Kuna mikutano ya kila siku na
viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo ili kuainisha maeneo ya makao ya
mashabiki "Eneo la Fan zone " katika Mikoa inayokaribia mechi za AFCON.
Mujahid alisisitiza kuwa Kamati ya Kuandaa
iliyoongozwa na Mhandisi Hani Abu Reda iliamua kuanzisha maeneo ya mashabiki
kama yale yaliyotokea katika Kombe la Dunia ili kurahisisha idadi kubwa ya
mashabiki waweze kutazamia michi, na kwamba uwanja huo hautaweza kupokea idadi
Kadhaa ya mashabiki.
Mujahid alisema kuwa kuchagua idadi ya maeneo katika
mikoa ya kairo, Suez, Ismailia na Port Said kutakamilika kwa kushirikiana na
Wizara ya Vijana na Michezo kwa ajili ya kuanzisha maeneo ya mashabiki katika
mikoa hiyo,ili kuwepo nafasi mbele ya mashabiki wa mataifa zinazoshiriki na
waweze kuhimiza timu zao kama yalivyotokea katika Kombe la Dunia pamoja na
kupatikan njia zote za raha katika
maeneo haya.
Comments