kuanza Uendeshaji “ chumba cha wanawake na kuzaa” kilichopewa kwa Burundi kutoka Misri


Bibi Abeer Basiuni Radwan “ Balozi wa Misri nchini Burundi” ameshuhudia shughuli za kuanza Uendeshaji wa chumba cha operesheni za  wanawake na kuzaa, kinachopewa kutoka Shirikisho la kimisri kwa Ushirikiano kwa ajili ya maendeleo.


 Na hicho kinazingatiwa kituo cha kipekee kinachohudumia mtaa fukara huu pembeni mwa Bugumbora “ mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi”. 


Na tukio hilo lilihudhuriwa na  mke wa waziri wa mambo ya nje wa Burundi” mwangalifu wa kituo cha matibabu na mkurugenzi wa kiufundi wa kituo”, mshauri wa kiutamaduni na kijamii kwa mtaa wa Gihosha, mwakilishi wa idara ya mtaa, na mwakilishi wa Meya wa Bugumbora. 


Pia Dokta Abeer Basiuni pamoja na wahusika waburundi wametafutia misaada ya matibabu inayotolewa kwa Shirikisho la kimisri kwa Ushirikiano kwa ajili ya maendeleo . 


Pia Balozi alifanya matembezi ya kuziangalia sehemu tofauti za kituo, na kusambaza misaada ya vyakula kwa wagonjwa na familia yao kupitia mifuko iliyochapwa khasa kwa jambo hilo yenye jina la Misri na picha ya Piramidi, pia kutolewa zawadi za kifarau na kumbukumbu kwa wahusika washiriki wote. 


Na kwa kuendelea mipango na misaada bure kwa jina  la Misri  ili kushirikiana na matatizo ya jamii ya Burundi khasa kwenye maeneo fukara yanayojazwa kwa wakazi , Balozi Dokta Abeer alipanga kundi la nne la misaada ya kimisri kwa juhudi za kibinafsi kupitia kutosheleza misaada Tani moja hivi ya vyakula , mingi toka kwake ni yenye asili ya kimisri , na kuisambaza kama msaada kwa jina la Misri kwa familia fukara zaidi zilizotolewa  kwa mji wa Bugumbora.


 Na hayo yote ni kwa mnasaba wa Uendeshaji wa chumba cha wanawake na kuzaa kilichopewa toka Misri  kwa kituo cha mtaa wa Gihosha unapopatikana pembeni mwa Bugumbora, pia kulingana na kampeni inayofanyikwa kwa Balozi ili kueneza chakula bora na umuhimu wa kutoa chumvi ya kimisri yenye Madini mnamo milo ya kila siku kama njia kuu ya Kinga kutokana na Maradhi yanayoenezwa zaidi nchini Burundi na eneo kwa ujumla, nayo ni kama Tezi inayosababishwa kutokana na Upungufu wa Madini.

Comments