Rais kwa vijana wa dunia : ugaidi ni kitu cha shetani kinachotumia akili na dini ili kuhakikisha faida za kisiasa
- 2019-12-17 10:53:39
Rais Abd Elfatah Elsisi akisisitiza kwamba ugaidi ni kitu cha shetani hatari yake kubwa ni matumizi ya akili na dini ili kuhakikisha malengo na faida za kisiasa ... Akiashiria kwamba ugaidi unawakilisha kifuniko cha malengo mengi ambayo nchi nyingi zinataka kuyafanya , na kutumia vifaa vyake dhidi ya binadamu na maendeleo yake ili kufikia malengo yake .
Rais El Sisi kwenye kikao cha ( changamoto za kisasa kwa Usalama na Amani za kimataifa ) siku ya jumapili 15/12/2019 baina ya matukio ya mkutano wa tatu wa vijana wa dunia unaofanyika mjini Sharmelsheikh amesema kwamba kupambana ugaidi huhitaji bidii kubwa ya kimataifa ... Akielezea umuhimu wa kusaidiana kufadhili nchi zinazokabili ugaidi , na akitaka uwepo wa msimamo mmoja dhidi ya nchi zinazoufadhili ugaidi akisema " tunapaswa kusema ukweli ".
Akiashiria umuhimu wa kufanya mkutano huo unaozingatiwa fursa ya kusikiliza wahusika mbalimbali kwa njia tofauti kwa maudhui moja , akielezea vijana ni makundi yaliyolengwa zaidi na ugaidi .
Rais akikaribisha wanaoshiriki kwenye kikao kwa njia kubwa na tofauti kwenye maudhui yanayohitaji kuzungumziwa , na akasema kwa vijana wa dunia kwamba lengo la mkutano huo ni kusikilizana na utofauti wa fikra na kuzungumzia maudhui moja ".
Comments