Karest : Mkutano wa vijana wa ulimwengu umeonyesha nguvu ya vijana katika utekelezaji wa maendeleo endelevu

Lueza Karest mwanaharakati wa haki za kibinadamu katika umoja wa mataifa, alisema kuwa malengo ya maendeleo endelevu sio ya kimataifa tu, lakini pia ni Ajenda kutoka wananchi wote na kwa ajili yao, ambapo inajumuisha kanuni za msingi, malengo yake yanafanana na malengo ya bara la Afrika katika Ajenda 2063.


Wakati wa hotuba yake katika mkutano wa "Hatua za maendeleo endelevu barani Afrika... Nafasi na Changamoto" miongoni mwa matukio ya jukwaa la vijana wa ulimwengu katika toleo lake la tatu chini ya uangalifu wa Rais Abd El fatah Elsisi, karest aliongeza kusema kwamba kuna nchi 147 zilitoa ripoti zake zenye elimu kwa jukwaa la kipekee linalofanyika kila mwaka katika umoja wa mataifa, ambapo serikali zote zilishiriki katika uandikaji wa ripoti hizo pamoja na wadau wanaohusika na mabadiliko katika maendeleo endelevu.


Karest aliendelea kwamba mwaka huu utashuhudia nchi 47 zitatoa ripoti zake, huku mwaka ujao unajumuisha nchi 49 ambazo zilisajili matakwa yake katika kutoa ripoti zake, nchi 16 miongoni mwa nchi zile kutoka bara la Afrika, na Misri ni mojawapo ya nchi zilizotoa ripoti yake mara mbili.


Pia alisema kuwa baadhi ya serikali ziliangliwa, ambapo serikali hizo zinashiriki pamoja na vijana na watoto kupitia kukagua ripoti zilizotolewa, ambapo Misri ilitoa ripoti iliyoonyesha ushiriki wa vijana katika utekelezaji wa maendeleo ya kudumu, na pia nchi ya Togo inaandaa kampeni za uhamasishaji kwa vijana wake katika nchi nzima.


Ametaja kuwa nchi zinapokuja ili kutoa ripoti za uhamasishaji kwa umoja wa mataifa, tunaona vijana wengi miongoni mwa ujumbe, akiashiria kuwa umoja wa mataifa una jukwaa la kimataifa ili kukagua utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya kudumu, na katika mwezi wa Septemba uliopita, mkutano mkuu ulifanyiwa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, mpaka viongozi wa ulimwengu waliomba kwa mkataba kuhusu malengo hayo.


Aliendelea kusema kuwa jukwaa la vijana litakalofanyika siku za kwanza na pili kutoka mwezi wa Aprili, mwaka ujao, litakuwa lenye nafasi ili kujadili serikali na nchi kuhusu mkataba wa kazi, akionyesha kuwa jukwaa la vijana wa ulimwengu nchini Misri limeonyesha nguvu ya vijana katika utekelezaji wa maendeleo endelevu 2030 pamoja na Ajenda ya 2063.

Comments