Wizara ya Vijana na Michezo inaendelea na shughuli za Mkutano wa Vijana wa Kiafrika "Uraia na Maendeleo"

Wizara ya Vijana na Michezo na Idara kuu kwa Bunge na Elimu ya kiraia zinaendelea na shughuli za Mkutano wa Vijana wa Kiafrika kuhusu "Uraia na Maendeleo" kwa kufanya vikao kadhaa vya mazungumzo na ushiriki wa wavulana na wasichana 100 kutoka nchi 20 za Kiafrika, ambazo ni "Morocco, Chad, Angola, Kenya, Zambia, Uganda , Malawi,Sudan, Algeria, Nigeria, Niger, Libya, Sierra Leone, Sudan Kusini, Somalia, Mauritania, Madagaska, Tunisia, na Ethiopia, "wakati wa kipindi cha Desemba hii13 hadi 19 katika Kituo cha Olimpiki huko Maadi.



Shughuli zilishughulika na kufanya kikao cha mazungumzo kwa Dokta Hassan Salama, profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Kairo, ambapo alisisitizia wakati wa mazungumzo na vijana wazo la serikali na nguzo zake za kimsingi ,Alizungumzia pia umuhimu wa kueneza haki, usawa, uhuru na demokrasia katika bara la kiafrika kwa sababu ni nguzo muhimu ya maendeleo, ambayo itafikia umoja wa kitaifa katika nchi zetu zote za Kiafrika ,vile vile aliwajadili Washiriki katika hali ya kisiasa katika kila nchi na alielezea kufanana na tofauti kati ya matumizi yao katika nchi za bara la kiafrika kunufaika kutokana na uzoefu uliofanikiwa na kujaribu kukabili changamoto, hasa kwa kuzingatia kukosekana kwa utulivu kwa nchi zingine za Kiafrika zinakabiliwa na ubaguzi, vita vya wenyewe kwa wenyewe na msimamo mkali, ambayo vijana wa kiafrika wanaita kutoa maoni yao juu ya matatizo yanayowakabili katika utekelezaji wa haki zao za kisiasa.



Salama alisisitiza kwamba kile wanachoota Inapatikana tu na uwepo nchi ya uraia inayoruhusu matumizi ya demokrasia ya kweli inayotegemea uwazi katika uhamishaji wa habari na uhuru wa kuchagua viongozi katika kile kinachoitwa nchi bora.


Comments