Udhamini kwa Jina la kiongozi "Gamal Abd Elnaser " kwa kuunga mkono viongozi wa vijana wa kiafrika.

Kulingana na yaliyotangazwa na Rais Abd Elfatah Elsisi mnamo matukio ya mkutano wa vijana wa dunia, pia kwa kutekleza uamuzi wake wa kuufanya mwaka wa 2019 uwe mwaka wa elimu, Ofisi ya Vijana wa kiafrika kwenye Wizara ya vijana na michezo imetangaza Udhamini wa "Nasser kwa uongozi wa kiafrika " mnamo kipindi cha 8 hadi 22 toka mwezi wa Juni ujao mjini Kairo.

 

Na kwenye kauli yake, Ofisi ya Vijana wa kiafrika ilionyesha kwamba Udhamini unawalenga vijana mia moja (100) kutokana na viongozi wakali wa nchi wanachama za Umoja wa kiafrika, kama watungaji maamuzi kwenye sekta ya kiserikali, watendaji kwenye sekta binafsi, vijana wa jamii ya kiraia, wakuu wa mabaraza ya kitaifa kwa vijana, wataalamu wa kufundisha kwenye vyuo vikuu, watafiti katika vituo vya tafiti za kimikakati na kimawazo, wanachama wa vyama vya kitaaluma, na Waandishi wa vyombo vya habari.

 

Ofisi ya Vijana wa kiafrika imefafanua kwamba Udhamini wa Nasser unazingatiwa mmoja wa vyombo vya uteklezaji wa mpango wa vijana milioni moja kwa kufikia mwaka wa 2021 - uliotolewa kwa ajili ya kuwawezesha na kuwaendeleza vijana barani Afrika.

 

Na Utoaji wa fomu ni kupitia linki ifuatayo.

( https://forms.gle/G8BcwbUKKaGnHXeZ8 )    

Comments