Makubaliano kati ya barua ya kimisri na DHL ili kupanga biashara ya badaaye ya kielektroniki barani Afrika
- 2019-12-18 11:14:41
Pembezoni mwa jukwaa la barua ya Afrika na kwa kuhudhuria Amr Talaat ,waziri wa mawasiliano na teknolojia na Nour Suliman ambaye ni, mkurugenzi mtendaji wa shirika la DHL Express kwenye Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini . shirika la DHL Express ambalo ni shirika la dunia lililoendesha huduma za kuelezea vifaa lilitilia saini makubaliano ya pamoja na shirika la kitaifa la barua ya kimisri,kwa ajili ya kusahili huduma za biashara ya kielektroniki barani Afrika kupitia kutoa huduma mpya ili kuharakisha mtindo wa usafirishaji wa haraka kwenda na kutoka bara la Afrika. Na kuweka Misri kama mhimili wa kimsingi wa maendeleo.
Na shirika hilo lilitangaza katika maelezo ya leo,kwamba makubaliano hiyo iliyotilwa kati ya mhandisi Asam El-Sagheir ambaye ni,mkurugenzi wa shirika la kitaifa la barua ya kimisri na Ahmed Al-Fangary ambaye ni,mkurugenzi mkuu wa DHL Express nchini Misri lengo lake ni kusahili na uratibu wa uundaji wa mkakati wa kielektroniki wa barua ya kimisri ili kuwa kama kituo cha shirika la kikanda la biashara ya kielektroniki kwa Afrika na pia kuunga mkono kazi za kibiashara ndogo na za kati nchini Misri. Ambapo pande hizo mbili zilikubali kushirikiana kwenye sekta ya usafirishaji,utoliaji na ushirikiano wa mnyororo wa ugavi kwa usafirishaji wa haraka wa barua za biashara ya kielektroniki kutoka na kwenda bara la Afrika.
Makubaliano yanaeleza yafuatayo :
Makubaliano yatatoa huduma za usafirishaji na usafirishaji nje tena katika kituo cha barua kwa kusanyiko kwenye bandari ya Kairo ya kimataifa na pia DHL kwa uzoefu wake kwenye Nyanja za biashara ya kielektroniki zitaunga mkono shirika la barua ya kimisri kwa kuendeleza operesheni iliyotakiwa na kutumia kituo cha barua nchini Misri kama kituo cha usambazaji kwa Afrika. Na shirika la barua ya kimisri litapata miundombinu iliyohitajiwa kwa shughuli hii. Ili kuwa kama masharti ya dunia kama katika nchi zingine. Lengo lake kuu ni kusahili operesheni za biashara ya kielektroniki kwa nchi za kiafrika kwenye bara la Afrika. Makubaliano hiyo inasema kuwa kutumia matawi ya barua ya kimisri yaliyowepo katika nchi na idadi yake ni matawi 4000 kama kituo cha kupokea bidhaa zilizopokelewa na mfano wa kusahili kwa wateja wa kampuni.
Nour Suliman ambaye ni,mkurugenzi mtendaji wa shirika la DHL kwenye Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini,alisema “tulifurahi kutilia saini makubaliano hiyo yatakayoimarisha mtandao wa DHL na kulisaidia katika kufikia maeneo mabalimbali katika Jumhuri ya Kiarabu ya Misri.”
Na kwa upande wa Ahmed Al-Fangry ambaye ni, mkurugenzi mkuu wa DHL nchini Misri alisema “ makubaliano hiyo ni kama msingi kwa kusahili biashra wa kielektroniki barani Afrika na kuweka Misri kama kituo kikubwa kwenye eneo na katika ramani ya sekta ya vifaa.”
Na kampuni hizo mbili zitachagua maeneo ya pekee ya barua ya kimisri na ambayo kupitia hiyo itatoa ujuzi uliohitajiwa kwa kampuni zinazobuka kwa kuuza kupitia internet kwa kiwango cha ulimwengu.
Comments