Waziri wa Vijana na Michezo anakutana na ujumbe wa Google kujadili njia za ushirikiano

Dokta Ashraf Sobhy , Waziri wa Vijana, alikutana na ujumbe wa Google katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kujadili njia za ushirikiano kati ya pande hizo mbili. 

Wakati wa mkutano, pande hizo mbili zilijadili uwezekano wa kunufaika na miundombinu ya Wizara ya Vijana na Michezo katika kutekeleza na kupanua mpango wa ujuzi kutoka Google, mipango ya Uwezeshaji wa watoto na vijana  kutoka kwa ujuzi wa dijiti, na utumiaji  wa kiusalama wa mtandao. 

Dokta Ashraf Sobhy  alisisitiza kwamba Wizara ya Vijana na Michezo ina vifaa vingi vya michezo na vifaa vya michezo vya vijana na vya kiwango cha juu zaidi cha kushughulikia hafla kubwa na mipango ya mafunzo inayofikisha  madarasa na Sekta zote za vijana wa kisri. 

Waziri wa Vijana na Michezo aliongeza kuwa Wizara inafanya kazi ya  kupanua msingi wa ushiriki wa vijana katika programu zake zinazohusiana na jinsi ya kutumia teknolojia ya dijiti na vyombo vya habari kwa njia salama, zenye uwajibikaji na ufanisi, na kuzuia hatari zinazohusiana na teknolojia, na hii ndio imani ya Wizara kwa umuhimu wa suala hilo ili vijana wa kimisri waweze kuendana na harakati za kiteknolojia za ulimwengu, akibainisha kuwa Wizara ya Vijana na Michezo inamiliki mipango mingi ya maendeleo na miradi ya kusaidia na kutunza vijana na kukidhi mahitaji yao, na katika mfumo wa kufanikisha maoni ya Wizara hiyo, ambayo inawakilisha mafunzo na kujenga uwezo na ujuzi wa vijana kama moja ya vipaumbele vyake muhimu.

Hii ilikuja kando ya kushiriki Mkutano wa Vijana wa  Ulimwengu,  unaokaribishwa  kwa mji wa Sharm El-Sheikh kutoka Desemba 14 hadi 17.

Comments