Jukwaa la kielektroniki la Kiarabu na kiafrika na kutoa mafunzo kwa vijana wa Euro-Kati juu ya uongozi ... Mapendekezo ya Vijana wa Dunia kwenye Mkutano
- 2019-12-18 13:10:50
Mapendekezo kumi yalitoka kutoka Jukwaa la Vijana wa Ulimwengu katika toleo lake la tatu, katika mji wa Sharm El-Sheikh, baada ya siku nne za majadiliano na semina iliyohudhuriwa na vijana kutoka nchi mbali mbali za ulimwengu, mbele ya Rais Abdel Fattah El-Sisi.
Mapendekezo yalikuwa kama ifuatavyo :
1. Kuzindua mpango wa kiafrika wa mabadiliko ya dijiti na ubora wa serikali kwa ushirikiano wa Umoja wa Afrika na Maabara ya Umoja wa kimataifa ya kiafrika kwa kuangalia Ubunifu wa Kiteknolojia.
2. Mwito wa kuzindua mpango wa kiafrika wa kupambana na Uharamia wa kielektroniki ili kulinda Taarifa muhimu ili kuwa kama ukuta wa kupambana majaribio ya kupenya kwa Dijiti.
3. Kuunda Jukwaa la kielektroniki la kiarabu na kiafrika kwa wanawake ambapo linajumuisha maktaba ya kielektroniki kwa masomo yote, karatasi za utafiti na ripoti kwa wanawake, likionyesha mafanikio ya wanawake, kuifanya jumla, na kusaidia katika njia za kuifadhili.
4. Mwito wa kuunda Kamati ya Euro-Kati ili kupambana na chuki ya kielektroniki, kuita Umoja wa Mataifa kuidhinisha Protokoli ya kimataifa ya kupambana na hotuba ya chuki, msimamo mkali na uonevu kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii na mtandao wa kimataifa.
5. Chuo cha Mafunzo cha Kitaifa nchini Misri kinaweka mifumo ya kiutendaji ya kuzindua mpango wa kiurais wa kufundisha vijana wa Euro-Kati kwa Uongozi.
6. tunaomba utekelezaji wa mpango wa Umoja wa Afrika 2021 ili kupatikana nafasi za kazi milioni moja
7. kutoa mpango wa kiutafiti kwa vyuo vikuu vya Afrika kwa ajili ya kuzingatia mbinu tofauti za Mapinduzi ya Viwanda ya Nne na kuangalia njia za kuyatumia ili kutatua shida za bara.
8 .Kuzindua mpango wa kusaidia watengenezaji wa "Blockchain" katika nyanja Tofauti ili kuunga mkono malengo ya maendeleo endelevu kwa ushirikiano na Jukwaa la World Youth Forum Lab lililozinduliwa kwa Mkutano wa Vijana wa Dunia ili kuhamasisha Vijana.
9 .Kuzindua mpango wa kimataifa kwa kichwa cha "Sanaa kwa ajili ya Utu " na kufanyika maonyesho ambapo wasanii hufanya kazi ya kuonyesha kitambulisho cha nchi zao tofauti na kuchora pia sura kutokana na nchi zao.
10. Kuanzisha vituo vya kubadilishana Taarifa kati ya nchi na kuita Taasisi kwa ajili ya kusaidia wavumbuzi ulimwenguni mwote.
Comments