Wizara ya Vijana na Michezo inaandaa mkutano wa Mwanamke mwafrika chini ya kauli mbiu "Afrika ni nchi moja"

 Leo , Chini ya uangalizi wa Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Wizara ya Vijana na Michezo inayowakilishwa kwa Idara kuu kwa Wanawake na Usawazishaji wa  nafasi hupanga Mkutano wa Mwanamke mwafrika (kiutamaduni - kimichezo- kiJamii - Burudani) baina ya jamii za Kiafrika ndani ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na jamii ya kimisri chini ya kauli mbiu "Afrika ni nchi moja", na hiyohutokeamnamo katika Kituo cha Vijana cha Al-Jazera.


Mkutano huo unakusudia kuimarisha kujihusisha kwa jamii za Kiafrika  pamoja na jamii ya kimisri na kubadilishana uzoefu na tamaduni, hii inakuja ndani ya shime ya serikali katika masuala ya Kiafrika na mwenendo mkubwa kuelekea bara la Afrika na inahusishwa na uwekaji wa Mheshemiwa Rais Abd ElFatah El-Sisi uongozi wa Umoja wa Afrika 


Mkutano huo ni pamoja na aya za kiutamaduni zilizowakilishwa katika mkutano wa utangulizi ulioitwa "Tuliwafanyeni watu na makabila ili mjuane ", kwa kuongeza aya za michezo zilizowakilishwa katika (mechi ya mpira wa miguu ya wanawake - mashindano ya michezo - michezo midogo- Zumba - uchoraji wa uso - Sehemu ya Sarakasi kwa watoto - wanasesere - uchorashaji wa Hina - Maonyesho na semina tofauti) pamoja na  aya tofauti za kisanii kwa sanaa ya kienyeji ya kimisri na kiafrika.


 Na inatarajiwa mahudhurio ya Msanii wa Nuba Hassan Abdel Majid na Bendi yake .

Comments