kwa ushiriki wa ujumbe wa Ofisi ya Vijana ya kiafrika ... Luxor inajiandaa kwa uzinduzi wa Al Afro-Arab katika toleo lake la kumi
- 2019-12-21 21:32:26
Shughuli za Mkutano wa 10 wa Vijana wa kiarabu na Kiafrika huko Luxor, unaoongozwa na Dokta Mamdouh Rashwan, zitaanza leo Jumamosi, kwa mahudhurio ya vijana 300 kutoka nchi za Kiarabu na Kiafrika, na kudhamini kwa kamati ya kiufundi ya Bodi la mawaziri wa Vijana na Michezo na ushiriki wa wizara za: Vijana na Michezo, Mazingira, Utalii, Umwagiliaji, Rasilimali za maji, Elimu ya juu, Utamaduni, Shirikisho la Kiarabu kwa Vijana na Mazingira, kituo cha Kuwaandaa viongozi, Baraza la Maji la Kiarabu na kampuni inayoshikilia maji ya kunywa na usafi wa mazingira.
Mkuu wa mkutano huo na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kiarabu kwa Vijana na Mazingira, Dokta Mamdouh Rashwan alieleza kwamba mkutano huo umefanyika katika wakati huu ni kama uthibitisho kwa matukio ya hivi karibuni yanaonyesha kuwa mtandao wa mahusiano ya kikanda unasonga kuelekea kuamsha ushirikiano kati ya nchi kama msingi mbadala wa mizozo kati yao, ambapo imekuwa wazi sana kwamba msingi wa migogoro hauleti maendeleo yoyote kwa maslahi ya umma ya nchi hizi, hasa kati ya vizazi vijavyo.
aliashiria kwamba Shirikisho linaamini katika jukumu bora ambalo vijana wanaweza kulichukua katika kuimarisha mahusiano haya ya kimataifa na kikanda, kwa kuzingatia maendeleo ya kiteknolojia katika uwanja wa mawasiliano, na kulingana na uwezo wa maingiliano ya vijana unaoendana haraka pamoja na matukio.
Aliongeza kuwa mkutano wa Vijana waarabu waafrika ni jukwaa la kikanda la kuonyesha na kubadilishana uzoefu katika kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu, na vikao tisa vimeshashikiliwa na vilijadili jukumu la vijana wa Kiarabu na Kiafrika kufikia malengo ya maendeleo endelevu , na kwa kuendelea kwa juhudi hizi, Shirikisho linaandaa mkutano wake wa kumi juu ya "Ushirikiano wa vijana waarabu waafrika".
Comments