kwa picha, uzinduzi wa shughuli za Mkutano wa Vijana waarabu waafrika huko Luxor
- 2019-12-23 13:06:41
Shughuli za mkutano wa kumi kwa Vijana waarabu waafrika zilizinduliwa kutoka mraba wa Abu Al-Hajjaj mbele ya Hekalu la Luxor huko mkoa wa Luxor .. ulioandaliwa kwa shirikisho la kiarabu kwa Vijana na Mazingira, kwa ushiriki wa vijana na wasichana 300 kutoka Misri na nchi kadhaa za Kiarabu na Kiafrika , kwa udhamini wa kamati ya kiufundi ya Bodi la mawaziri waarabu wa vijana na michezo , na kwa Ushiriki wa Wizara za Vijana na Michezo na, Mazingira, Utalii, Umwagiliaji na Rasilimali za Maji, Elimu ya Juu, na Utamaduni, kwa mahudhurio ya vijana wa vyuo vikuu vya kimisri , Kiarabu na Kiafrika na wataalamu wa taasisi na mashirika ya Kiarabu na ya kikanda yanayohusika.
Dokta Mamdouh Rashwan, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Katibu Mkuu wa shirikisho la kiarabu kwa Vijana na Mazingira, alisema katika kauli yake ya ufunguzi kwamba mkutano huo unakuja mnamo wakati muhimu, hasa na shime ya Misri katika fursa za uwekezaji, kuhifadhi jamii na kuikinga kutoka kwa uzushi na ugaidi, na kusonga mbele katika kuendeleza maendeleo na kuendeleza vijana na kukuza uwezo wao.
Rashwan ameongeza kuwa shirikisho hilo liliandaa mkutano wake wa kila mwaka wa vijana waarabu waafrika kwa kuzingatia matokeo ya mikutano ya kimataifa na kutangazwa kwa Jukwaa la Vijana wa Ulimwengu, lililofanyika kwa Misri chini ya uangalifu wa Rais wa Jamhuri, na mji wa Aswan, mji mkuu wa vijana wa Kiafrika kwa mwaka wa 2019 .. akiashiria imani ya Shirikisho katika jukumu bora ambalo vijana wanaweza kulichukua Katika kuimarisha mahusiano haya ya kimataifa na kikanda, wakati wa maendeleo ya kiteknolojia katika uwanja wa mawasiliano, na hayo yote ni kwa sababu ya uwezo wa maingiliano wa vijana unaoendana haraka pamoja na matukio.
Dokta Mamdouh Rashwan alisema kuwa mkutano huo utajadili masuala yanayohusu uwezeshaji wa vijana na uundaji wa fursa tofauti na nzuri za ajira, masuala ya maji katika ulimwengu wa Kiarabu ,njia za kuyapambana na kutatua shida zake , kujenga uchumi wa taarifa ndani ya vijana, na kukuza ujuzi .. Akisisitiza umuhimu wa uelewa wa maji ya Kiarabu na Kiafrika kwa mtazamo wa maendeleo endelevu, na masuala ya ugaidi, maendeleo na kuunda uchumi wa taarifa ndani ya vijana.
Kwa upande wake, Abdel-Moneim El-Shaaery, Waziri mwakilishi , Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kwenye chuo kikuu cha mataifa ya kiarabu alithibitisha kwamba mkutano huo ni nafasi nzuri ya kubadilishana uzoefu na kusaidia vijana kukabiliana na changamoto na kuwasiliana ili kuhakikisha maendeleo endelevu .. akithamini kuanzisha vikao kama hivyo kwa ajili ya kuthibitisha mazungumzo yenye ujumbe kupitia ujumbe kwa ulimwengu kuwa vijana ni watetezi wa Amani na wanakataa Ghasia na Msimamo mkali .
Al-Shaaery alifikisha salamu za Katibu Mkuu wa chuo kikuu cha nchi za Kiarabu kwenye mkutano huo katika ujumbe unaothibitisha umuhimu wa kushika mkutano huo mnamo kipindi hicho muhimu kwa ajili ya kujadili masuala ya Kiarabu na Kiafrika.
Kwa upande wake, Dokta Ahmed Al-Sahem, mwakilishi wa Wizara ya Vijana na Michezo, alisema kuwa wizara hiyo iko tayari katika kipindi kijacho kuunda kada za vijana kupitia mawasiliano nao kupitia kwa idara za vijana na michezo, taasisi za jamii ya kiraia , njia za kielektroniki za kisasa na utekelezaji wa vikao vingi vya vijana.
Kwa upande wake, Meja Jenerali Mohamed Yahya, Mwenyekiti wa kampuni ya Maji na Usafi wa kiafya huko Luxor, alithibitisha kwamba mkutano wa leo ni moja wapo ya majukwaa muhimu ya kuelezea maoni na tamaduni tofauti ... akithibitisha shime ya kampuni hiyo ya kushiriki katika mkutano muhimu huo wa kila mwaka kupitia semina za utangulizi kwa umuhimu wa kuhifadhi maji kama suala kuu , inapaswa kukuza uhamasishaji wa vikundi vyote, hasa vijana, kwa sababu malengo ya maendeleo yatahakikishwa ila kwa kuwekeza katika maendeleo ya wanadamu.
Kwa upande wake, Dokta Mohamed Abd El Kader, Naibu wa Gavana wa Luxor, alisisitiza umuhimu wa mkutano huo kama nguzo muhimu ya mawasiliano kati ya vijana na vizazi tofauti ... akiashiria kuwa moja ya nguzo za mafanikio katika nchi yoyote ni upatikanaji wa masuluhisho na mitazamo kwa masuala kadhaa .
Abd El Kader ameongeza kuwa mkutano huo ni nafasi muhimu kwa mawasiliano ya nchi na tamaduni tofauti , hasa ya kiafrika, pia ni nafasi ya kuwasiliana Ustarabu ambapo Misri imeupitia, na akiashiria kuwa Misri imepiga hatua kubwa katika suala la uwezeshaji wa vijana, hasa mnamo kipindi kilichopita na kuwepo kwao mkubwa katika maeneo yote ya uongozi na mikutano.
Comments