Alhamisi,katika hoteli fulani katika jiji la Kairo ilishuhudia shughuli za mkutano wa waandishi wa habari kwa kutangaza kwamba Misri ilishinda Michezo ya kwanza ya Kiafrika kwa Olimpiki Maalumu ya Misri 2020 chini ya uangalifu wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri.
Mkutano huo wa waandishi wa habari ulihudhuriwa na Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Nevin Al-Kabbaj, Waziri wa Mshikamano wa kiJamii ,Mhandisi Ayman Abdel Wahab, Mwenyekiti wa Kamati kuu ya Kuandaa Michezo, Rais wa kikanda wa Michezo ya Olimpiki ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, na Charles Nyambi, Rais wa kikanda wa Olimpiki Maalum ya Afrika.
Hussein Fahmy, Balozi wa Olimpiki Maalum ya Kimataifa, Mhandisi Hani Mahmoud , Rais wa Olimpiki Maalum ya Misri, Maher Al-Adawi, Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Masuala ya Kiafrika, na ushiriki mwema kutoka kwa mchezaji Ibrahim El-Khouly na mchezaji Maryam Adel kutoka Olimpiki Maalum ya Misri kwa ushiriki wa idadi kadhaa ya waandishi wa habari na wafanyikazi vyombo vya habari katika taasisi tofauti.
Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Ashraf Sobhy, alitangaza wakati wa hotuba yake kwamba Misri ilishinda shirika la Michezo ya kwanza ya Kiafrika kwa Olimpiki Maalum, ambayo itafanyika chini ya uangalifu wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri.
Sobhy alisisitiza kwamba alikuwa akiota tangu wakati huo kuandaa hafla kama hiyo nchini Misri, ambayo ilifanikiwa sasa, akitamani kuandaa mashindano ya kutofautisha kutoka mwanzo hadi mwisho, kwa sababu kila wakati Misri inakuwa na uwezo wa kuandaa mashindano haya makubwa barani Afrika.
Wakati huo huo, Waziri wa Mshikamano wa kijamii Nevine El Kabbag alielezea furaha yake kuwa Misri ilishinda michezo hii muhimu, ambayo inaambatana na urais wa Rais Abdel-Fattah El-Sisi wa Jumuiya ya Afrika, na kusisitiza kwamba Wizara ya Mshikamano wa Jamii inaona umuhimu mkubwa kwenye faili ya watu wenye ulemavu nchini Misri.
akitamani kuwepo ushirikiano wa pamoja kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Mshikamano wa kijamii mnamo kipindi kijacho cha kutumikia walemavu na kuwajihusisha katika jamii.
Kwa upande wake, Ayman Abdel Wahab, Rais wa kikanda wa Olimpiki Maalum ya kimataifa, alisisitiza kwamba udhamini wa Rais El Sisi wa Michezo ya kwanza ya Afrika kwa Olimpiki Maalum ni ujumbe wa kibinadamu kwa ulimwengu wote, akielezea furaha kubwa kwamba michezo ya kwanza ya Afrika itafanyika kwenye nchi ya Misri, ambayo pia ilishuhudia michezo ya kikanda ya kwanza kwa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Mwaka wa 1999.
Kama Charles Nyambi, Rais wa kikanda wa Olimpiki Maalum ya Afrika alisema, "nina furaha kubwa sana kushikilia michezo ya kwanza ya Kiafrika kwenye ardhi ya ustaarabu wa zamani zaidi wa mwanadamu, na akasimulia hadithi ya mchezaji wa Kiafrika ambaye alikuwa akiumia kutoka kutengwa na uzembe katika makambi ya wakimbizi hadi alipoingia ulimwengu wa Olimpiki Maalum na maisha yake yamebadilisha kuwa bora.
Wakati mkutano huo uliofanyika wanariadha Maalum wa Olimpiki, Maryam Adel, na Ibrahim Al-Khouli, watazamaji walishangazwa na walichokisema.
Ni muhimu kutaja kuwa Misri itakuwa mwenyeji wa Michezo ya kwanza ya Kiafrika kwa Olimpiki Maalum chini ya uangalifu wa Rais Abd El Fatah El-Sisi katika michezo minne, nayo ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, Bochi, na michezo ya nguvu, kuanzia tarehe 23 hadi 31 Januari 2019.
Comments