Mwishoni mwa shughuli za Mkutano, Vijana wa Al-Afroubi wanampongeza Rais El-Sisi kwa msaada wake wa kudumu kwa vijana

Vijana wa Jukwaa la 10 la Afro-Arab walimsalimiana na kumshukuru Rais Abdel Fattah Al-Sisi kwa msaada wake wa kudumu kwa vijana, mwishoni mwa shughuli zake katika Kituo cha Utamaduni cha Afrika "makumbusho ya Nili hapo awali" huko Aswan, lililofanyika chini ya kichwa cha "Ushirikiano wa Vijana wa kiarabu -Kiafrika" kwa mahudhurio ya wakilishi wa Wizara ya Vijana na Michezo, wataalamu wa umoja na wakuu wa ujumbe wa kiarabu na kiafrika. pamoja na ushiriki wa Vijana na wasichana311 kutoka nchi 33 za Kiarabu na Kiafrika ambao uliendelea kwa wiki hii katika mikoa ya Luxor na Aswan kwa udhamini wa Chuo kikuu cha Nchi za Kiarabu.

Dokta. Mamdouh Rashwan, Rais wa Baraza hilo, alisisitiza kwamba mapendekezo ya Mkutano huo utawasilishwa kwa mawaziri wa vijana wa Kiarabu katika mkutano wao ujao kwenye Jumuia ya Nchi za Kiarabu, na pia alishukuru Ofisi ya vijana waafrika kwa jukumu la ke la kuwaita washiriki waafrika.

Kwa upande wake Mhandisi. Rifaat Ismail, Mwenyekiti wa Bodi la Wakurugenzi wa Kampuni ya Maji na Usafishaji wa maji huko Aswan, alisema kuwa kushughulikia utumiaji mzuri kwa maji ni moja wapo ya mihimili muhimu ambapo kampuni inayoshikilia inaiweka kati ya vipaumbele vyake, na inatafuta kufanikisha hilo kwa kuzingatia sehemu ya kiufundi iliyowakilishwa katika kugundua njia ya kuvuja na viunganisho na uzoefu mpya kwa utumiaji. Maji, na kukuza rasilimali za maji kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya Utamu wa Maji, pamoja na vipande vilivyopatikana na kuifanya vipatikane kwa watumiaji ili kuwa na matumizi mazuri.

Dokta Ehab Abdel Aziz, mwakilishi wa UNICEF, ameongeza umuhimu wa kushirikiana na Shirikisho la Kiarabu la Vijana na Mazingira na Kampuni ya kushikilia ya Maji na Usafishaji wa Mazingira kuhusu masuala ya maji na kukuza Uelewa, na uliowakilisha kwa mkutano huo kwenye mazungumzo ya vijana kutoka nchi tofauti za Kiarabu na Kiafrika juu ya jinsi ya kusimamia masuala ya maji na ubunifu wa kutafuta masuluhisho ya ubunifu kwa changamoto zinazopo, kutoa vyanzo mbadala vya maji na Utumiaji bora.

Kwa upande wake, Naibu Muhammad Khalifa alithibitisha kwamba mkutano huo ni moja wapo ya vikao muhimu vilivyofanyika nchini Misri ukiwa kama utekelezaji wa mielekeo ya Rais Abdel Fattah Al-Sisi kwa kuwasaidia vijana kwa kuanzisha mikutano hii ambayo ina sura nyingi za kitamaduni, kisiasa na kijamii ... akisisitiza hitaji la kufanya kazi ili kuwawezesha vijana waarabu kiuchumi, kisiasa na kijamii ili Kuwa tayari kwa changamoto zinazozikabili nchi zote za Kiarabu.

Dokta Ahmed Al-Sahem, mwakilishi wa Wizara ya Vijana na Michezo, alisisitiza juu ya shime ya Wizara katika mipango ya uwezeshaji wa vijana, hasa kama kujenga wanadamu ni muhimu zaidi kuliko kujenga jiwe, wakizingatiwa kuwa vijana ndio wajenzi wa siku zijazo. Al-Sahem alionyesha kuwa ushirikiano kati ya Wizara, Shirikisho la Kiarabu kwa Vijana na Mazingira, Kampuni ya Maji ya Usafishaji wa Mazingira, UNICEF na nyenginezo zinazoshiriki katika Mkutano wa 10 wa Vijana wa Afro-Arab ni kielelezo cha malengo ya maendeleo endelevu katika kufanikisha ushirikiano .pia aliisifu miji ya vijana huko Luxor na Aswan na ushirikiano wao mzuri wakati wa mkutano huo.

na wakati wa kuhitimisha sherehe hiyo , Shirikisho la Kiarabu kwa Vijana na Mazingira liliziheshimu taasisi zilizoshirikiana kufanikiwa mkutano huo pia liliheshima ujumbe ulioshiriki kama ujumbe wa Palestina, Morocco na Algeria zipangazo mkutano na hitimisho la sherehe hii ilikuja pamoja na maonyesho ya Muziki kwa Bendi ya CHOKI kwa sanaa za kienyeji za kinoba.


#AfroArabForum #AfroArab10 #الافروعربى #AfricanYB

Comments