Shirikisho la mpira wa wavu : mahudhurio ya fainali zitakazofikisha Tokyo 2020 kupitia (tiketi yangu)

Mwenyekiti wa shirikisho la Kimisri Ia mpira wa wavu, Ahmed Abd Aldayem ametangaza kuwa kuna itifaki pamoja na kampuni ya (tiketi yangu) kwa ajili ya mahudhurio ya mashabiki na familia ya mpira wa wavu katika mechi zitakazofikisha  Olimpiki kwa bei thabiti (paundi 25).


Ukumbi uliofunikwa katika uwanja wa kimataifa wa Kairo, ukumbi wa namba 2 utakaribisha mechi hizo mnamo kipindi cha tarehe 6 hadi 12 Januari.


Kura ya mechi za fainali za Kiafrika kwa mpira wa wavu ilifanyika, ambapo timu ya kitaifa ya Misri ya kwanza itaanza mechi zake katika fainali hizo mbele ya timu ya kitaifa ya Algeria kisha itacheza mbele ya timu za kitaifa za Ghana, Tunisia na Cameron kwa mfululizo mnamo kipindi cha tarehe 7 hadi 11, mwezi wa Januari ujao, na siku ya 10 Januari itakuwa mapumziko kwa timu ya kitaifa ya Misri.

Comments