Mchezaji mmisri Soraya Muhammad ni miongoni mwa wachezaji 10 bora zaidi wa mpira wa kikapu ulimwenguni
- 2019-12-31 13:03:38
Baraza la Wakurugenzi wa Shirikisho la la kimisri la Mpira wa kikapu, liliyoongozwa na Dokta Magdy Abu Freikha, lilipokea habari ya kuchaguliwa Soraya Muhammad mchezaji wa timu ya kitaifa ya kimisri na Klabu ya Al-Ahly, miongoni mwa wachezaji 10 bora zaidi wa mpira wa kikapu 3x3 ulimwenguni na shirikisho la kimataifa la Mpira wa Kikapu.
Shirikisho la Kimataifa lilisifu mchezaji huo baada ya kufanikiwa kupata alama nyingi hadi ikaelezewa kama Kelopatra mpya.
Kwa kuzingatia kiwango kilichowasilishwa na mchezaji huyo na klabu yake, Klabu ya Morocco ya Meknesi iliwasilisha ombi kwa klabu ya Al-Ahly ikiomba kukopa mchezaji huyo katika Mashindano ya kiarabu kwa klabu , lakini Shirikisho lampira wa kikapu la kimisri lilikataa kwa sababu ya ushiriki wake na mechi na timu ya wanawake.
Ni muhimu kutaja kuwa Soraya Muhammad alitawazwa na Klabu ya Al-Ahly kwa medali ya shaba ya Mashindano ya kiafrika ya klabu za Wanawake, iliyofanyika nchini Misri, na ushiriki wa Al-Ahly na Sporting, na timu ya Sakandry ilikuwa ya nne.
Mchezaji huyo pia alitawazwa na klabu yake katika mashindano ya ligi, kwenye mechi pamoja na Al-Jazira, baada ya kushinda kwa alama 82-60 katika marudio ya fainali ya mashindano, uliyofanyika kwenye Ukumbi wa Vijana na Michezo katika mji wa 6 Oktoba .
Bodi la Wakurugenzi linasistiza kuwa uteuzi wa Soraya Mohamed unaongezewa kwa mafanikio mazuri ya mpira wa kikapu wa kimisri mnamo 2019.
Comments