"Misri Afrika .. Utamaduni wa Utofauti " kauli mbiu ya kikao cha 51kwa Maonyesho ya Kairo ya kimataifa kwa kitabu .. Senegal ni mgeni wa heshima
- 2020-01-01 11:21:58
Wizara ya Utamaduni ya kimisri ilichagua kauli mbiu ya " Misri Afrika .. Utamaduni wa Utofauti" kuwa kichwa cha kikao cha mwaka huu. Pia ilitangaza kwamba mgeni wa heshima ni Jamhuri ya Senegal, na mhusika wa maonyesho hayo ndiye mfikiri mtaalamu mkubwa marehemu Jamal Hamdan.
Wizara ya Utamaduni ya kimisri na Mamlaka kuu kwa kitabu inajiandaa kwa maandalizi ya mwisho ya shughuli za Maonyesho ya Kairo ya kimataifa ya kitabu , kikao chake cha 51, kitakachofanyika kutoka Januari 22 hadi Februari 4 2020 katika Kituo cha Mikutano na Maonyesho za Kimataifa huko Kairo Mpya.
mnamo kipindi cha maonyesho cha awali, hafla kadhaa za semina za zamani na semina zitapandishwa, pamoja na kongamano lililofanyika mnamo 1988 na mshairi marehemu Nizar Qabbani.
Kati ya shughuli mpya katika hafla za mwaka huu ni mpango wa mabalozi wa maonyesho, ambapo msanii mjuzi mmisri Samiha Ayoub alichaguliwa kama balozi wa maonyesho ya kitabu 2020.
Idadi kubwa ya nyumba za kuchapisha ulimwenguni mwote na idadi kubwa ya wasomi na waandishi hushiriki katika maonyesho hayo, ambapo semina kadhaa zinafanywa na umma.
Katika muktadha wa maandalizi yanayoendelea na Senegal, mgeni wa heshima katika Maonyesho ya Kairo ya kimataifa ya kitabu, Balozi wa Misri huko Dakar Noha Khedr , alipokea washiriki wa ujumbe wa Senegal, mwakilishi wa Wizara ya Tamaduni na anayeandaa ushiriki wa Senegal katika maonyesho.
Comments