Wizara ya Vijana inatekeleza ruwaza ya mfumo wa kuiga Umoja wa Afrika chini ya Uangalifu wa Waziri Mkuu
- 2020-01-01 16:20:12
Wizara ya Vijana na Michezo ilitangaza utekelezaji wa ruwaza ya mfumo wa kuiga Umoja wa Afrika mnamo kipindi kijacho chini ya uangalifu wa Dokta Mustafa Madbouly, Waziri Mkuu na Kameshina ya Umoja wa Afrika huko Addis Ababa.
Hatua ile inazingatiwa ya kwanza ya aina yake kwa "mfumo wa kuiga" kupokea udhamini wa taasisi mbili kutoka kwa Baraza la Mawaziri la kimsri na Kameshina ya Umoja wa Afrika wakati wa Urais wa Rais Abd El-Fatah El-Sisi kwa Umoja wa Afrika, na wakati wa kuhangaika kwa taasisi zote za nchi ya kimisri kwa kuimarisha Ushirikiano wa kiafrika wa pamoja, inakuja pia ikifuatilia mielekezo ya uongozi wa kisiasa kuelekea kutoa aina zote za Uwezeshaji na mafunzo kwa vijana, hasa yanayohusu Afrika.
Mfumo wa kuiga wa Umoja wa Afrika ni mojawapo ya mifumo ya kiuteklezaji kwa mapendekezo ya Mawaziri waafrika wa Vijana na Michezo na Utamaduni, iliyoandaliwa kwa Ushirikiano na Ofisi ya Vijana ya Kiafrika katika Wizara ya Vijana na Michezo wakati wa mikutano ya kikao cha tatu cha kiufundi huko Algeria kutoka 21 hadi 25 Oktoba 2019, ambapo ilisisitiza uhamisishaji wa mifumo ya kuiga Umoja wa Afrika na shughuli zengine. hivyo ndivyo, vinavyofanya kazi kwa kueneza dhana ya umoja wa Kiafrika kati ya vijana ndani na nje ya taasisi za kielimu ili kuongeza Ushirikiano, na kuangalia mchakato wa kuamua kwenye Umoja wa Afrika.
Na hivi karibuni, Wizara ya Vijana na Michezo iliweza kupata Dhamana ya Kameshina ya Umoja wa Afrika kwa mfumo wa Kuiga. Na wakilishi wa Ofisi ya Vijana ya Kiafrika walishiriki kwenye kozi ya mafunzo ya uzinduzi wa mifumo ya kuiga Umoja wa Afrika Barani.
Comments