Ashraf Sobhy anaongoza Mkutano Mkuu wa Ofisi ya kiutendaji kwa Baraza la Mawaziri waarabu wa vijana Michezo

Mkutano wa Ofisi ya kiutendaji wa Baraza la Mawaziri waarabu wa Vijana na Michezo ulianza asubuhi hii katika kikao chake cha 64 kilichoongozwa na Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo na mkuu wa Ofisi ya kiutendaji kwa Mawaziri waarabu  wa Vijana na Michezo, kwa mahudhurio ya Mawaziri waarabu  wa Vijana  na Michezo, wanachama wa Ofisi ya kiutendaji.


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo na Mkuu wa Ofisi ya kiutendaji wa Mawaziri waarabu wa Vijana na Michezo, aliwakaribisha mawaziri nchini Misri, akisisitiza umuhimu wa sera ya jumla kwa uwanja wa vijana na michezo katika ofisi ya kiutendaji inayojadiliwa ili kuwahudumia vijana na masilahi zao, na kuendelea kuainisha mifumo ya hatua za shughuli , akiongeza kuwa kuna kipaumbele kikubwa kinachoambatanishwa na mawaziri  waheshemiwa ili kuratibu kati ya nchi za Kiarabu katika nyanja za vijana na michezo na hufanya kazi kutekleza.


Sobhy alisisitiza kwamba maoni ya jumla kwa Rais mheshemiwa, Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, yanayolenga kuinua na kuendeleza shughuli zote za vijana na michezo ambazo hutolewa kwa vijana wetu katika ulimwengu wa Kiarabu, ili kukabiliana na changamoto zote.


Maoni haya yalithibitishwa na mawaziri waheshemiwa na wanachama wa Ofisi ya kiutendaji, waliomshukuru Rais wa Jamhuri, Abd El Fatah El-Sisi, kwa msaada wake usio na kikomo kwa shughuli zote za Ofisi ya kiutendaji kwa Mawaziri  waarabu wa Vijana na Michezo, waliosifu maoni hayo ya kimkakati, ambayo ni pamoja na shughuli za Kairo, mji mkuu wa vijana wa Kiarabu, ambao ulijumuisha shughuli na mipango kadhaa. Hiyo ilitekelezwa kwa vijana wote wa Kiarabu, akizingatia mwendelezo wa shughuli hizo, akisifu shughuli zilizotekelezwa kwa sasa nchi ndugu Tunisia kama ilivyo sasa mji mkuu wa vijana wa Kiarabu, halafu zitahamishwa kwa miji mingine ya nchi za Kiarabu.


Wakati  Bibi Haifa Abu Ghazaleh, Katibu Mkuu Msaidizi wa Shirikisho la Kiarabu na Mkuu wa Sekta ya Masuala ya kijamii, akifikisha salamu za Bwana Ahmed Aboul Gheit, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kiarabu kwa Mawaziri waheshemiwa , akiongeza umuhimu wa kufanya shughuli mbali mbali za vijana na michezo na kwamba shughuli zinazofanywa ziwe na faida kubwa kwa vijana, na kufikia sekta kubwa zaidi ya vijana  kama inavyowezekana.


Mkutano huo ulijadili mihimili na shughuli kadhaa zilizofanywa wakati wa kikao hiki katika nchi kadhaa za Kiarabu, pamoja na mpango wa mkurugenzi mtaalamu wa uuzaji , Tunisia, mji mkuu wa vijana wa Kiarabu, Jukwaa la Vijana la Waarabu huko Tunisia, Mkutano wa saba wa Vijana Waarabu huko Budapest, mkutano wa kiarabu kwa Vijana " mabalozi wa Amani" Mkutano wa Vijana waarabu waafrika , na kikao cha upangaji na utawala cha 18  huko Morocco


Wajumbe wa Halmashauri Kuu walikubaliwa pia kwa makubaliano kupeana shirika la Michezo ya Kiarabu ya 2021 kwa nchi ya Iraqi

Katika muktadha unaohusiana, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Mwenyekiti wa Ofisi ya kiutendaji ya Mawaziri wa Vijana na Michezo, aliwaalika mawaziri na wajumbe wa Ofisi ya Watendaji wakuu kuhudhuria mkutano huo "Wadau wa Vijana Kutumia Teknolojia ya Taarifa na Uhusiano wake wa kupambana naUgaidi " unaoandaliwa kwa Wizara ya Vijana na Michezo, na unafanyika kwa uratibu na ushirikiano na Jumuia ya Nchi za Kiarabu mnamo  Januari 4 hadi Januari 6 katika makao makuu ya chuo kikuu kwa mahudhurio ya kikundi cha mawaziri  waheshemiwa na wakilishi wa ujumbe wa kidiplomasia, na kikundi cha wasomi, waandishi na wataalamu katika masomo ya kisiasa na masuala ya kidini.


 Mkutano huo unajumuisha vikao vinane vya majadiliano kuzungumzia kundi la mihimili mikuu lililowakilishwa katika "jukumu la taasisi za kidini katika kupambana na ugaidi na msimamo mkali, familia, elimu na vyombo vya habari kama msingi wa kutega Msimamo mkali , Teknolojia kati ya kuhudumia na kukabiliana na ugaidi, ugaidi na vijana na vifaa vya kuendeleza uwezo wa kiteknolojia katika kupamba msimamo mkali na ugaidi ,"  Jukumu la nguvu laini katika kukabiliana na ugaidi na msimamo mkali, jukumu la taasisi zaJamii ya kiraia katika kukabiliana na ugaidi na msimamo mkali, "pamoja na  kuonyesha harakati maarufu za vijana zinazoshiriki katika matukio za mkutano huo.

Comments