Kufungua Mlango wa kuomba kujitolea ili kushiriki katika kupanga michezo ya kiafrika kwa Olimpiki

Wizara ya vijana na michezo inatangaza wakati wa kufungua mlango wa kuomba kwa vijana wanaojitolea ili kushiriki katika kupanga michezo ya kiafrika kwa Olimpiki  inayofanyika mjini Kairo mnamo kipindi cha 23 hadi 31 mwezi wa kwanza 2020 kwa ushiriki wa nchi 42 za kiafrika zinashindana katika michezo ya ( michezo yenye nguvu , mpira wa miguu , mpira wa kikapu na Mchezo wa Bochi) 


Na kuna sharti kwa wanaojitolea nazo ni 

wasiwe na shughuli yoyote mnamo wakati wa olimpiki , ustadi wa lugha za ( kiarabu , kiingereza , kifaransa ) na uwezo wa kutumia kompyuta na kuchora kwa ubuni pamoja na uchaguzi wa kikundi cha wanaojitolea wanaohusika katika huduma za kiutabibu.


Na mahojiano yanafanyikwa katika kituo cha elimu ya kiraia kwenye Aljazira kinachohusu wizara ya vijana na michezo na kinachopo katika mwisho wa barabara ya mnara wa Kairo na hii ni kama ifuatavyo :


Siku ya alhamisi 9 mwezi wa kwanza 2020 kutoka saa 10 hadi saa 3 jioni.


Siku ya Ijumaa 10 mwezi wa kwanza 2020 kutoka saa 8 aldhuhuri hadi saa 3 jioni. 


Siku ya jumamosi 11 mwezi wa kwanza 2020 kutoka saa 10 hadi saa 3 jioni.


Na lazima kuandika maelezo yanayotakiwa katika fomu ya kibinafsi kwa wanaojitolea na kuja katika mahojiano pamoja na sura ya kibinafsi na nakala ya kitambulisho .

Comments