Waziri wa Vijana na Michezo anashuhudia uzinduzi wa Mkutano wa mipango ya Vijana kwa kutumia Teknolojia ya Taarifa na uhusiano wake kuondokana na Ugaidi kwenye Jumuiya ya Nchi za Kiarabu

  Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishuhudia mkutano huo "Hatua za kuharakisha  za Vijana Kutumia Teknolojia ya Taarifa na Uhusiano wake na kuondokana Ugaidi" chini ya usimamizi wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, itakayofanyika Januari 4 hadi Januari 6 katika makao makuu ya chuo kikuu kwa mahudhurio ya kikundi cha mawaziri na wakilishi wa ujumbe wa  kidiplomasia, na kikundi cha wasomi, waandishi na wataalamu Katika masomo ya kisiasa na masuala ya kidini.

 Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alianza hotuba yake kwa kufikisha salamu za Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa washiriki wote, akionesha kwamba mkutano huo unashughulikia  uangalifu wa wizara hiyo ya kuboresha michango ya vijana katika nyanja mbalimbali za ujenzi na maendeleo, pamoja na suala la kupambana na ugaidi na msimamo mkali katika mkutano huo uliofanyika chini ya kauli mbiu.  Mipango ya vijana kwa  kutumia Teknolojia ya Taarifa na uhusiano wake kuondokana ugaidi.

 Aliashiria kwamba mkakati uliopitishwa na uongozi wa kisiasa wa kimisri katika suala hili, uliotegemea sana kuchambua mambo ya kisiasa , kuweka sheria, na kurekebisha mifumo mingi inayohusiana na kuhesabu ugaidi na msimamo mkali, ilikuwa na uungaji mkono kwa jamii ya kimataifa, ambayo mwishowe iligundua hitaji la kudhibitisha juhudi na ushirikiano wa nchi zote, mashirika, taasisi na watu wote kuondoa  jambo baya hilo, ambayo ilifanya Misri kuwa mwenye uzoefu, uongozi na kipaumbele mbele ya mambo yote ya kigaidi na msimamo mkali, na akasisitiza kwamba vijana wamisri hawakuwa mbali na matukio haya, lakini michango yake ilikuwa wazi na haivumilii machafuko au tafsiri kuhusu suala hilo. basi mwanzoni tulikuwa na waliojitolea nafsi yao toka vijana wa Misri kutoka kwa wanajeshi wa Kimisri na polisi hodari katika nyanja zote za mapigano, na hapo ndipo ndugu zao kutoka kwa vijana wa kike na wasichana katika nyanja zote za kazi za kiraia walikuwa na jukumu la kuunga mkono na kusaidia kwa wao kwa kutumia njia tofauti , pamoja na hatua za kuharakisha za vijana kutegemea na utumiaji wa Teknolojia ya Taarifa.

 Aliendelea kwa kusema kwamba kwa kuzingatia maagizo ya Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, tumewahi kwamba kuheshima jukumu la vijana na kuanzisha michango yao katika nyanja mbalimbali ni jambo la lazima na muhimu katika nyanja zote za ujenzi na maendeleo, hasa zile zinazohusiana na kupambana na janga la misimamo mikali na ugaidi.  kwa imani yetu kuwa wao ni nguvu ya ubunifu, ambao una uwezo unaostahili kwa sifa kamili kwa kuchukua jukumu na kushiriki kikamilifu katika kupanga  hali ya kisasa na kujenga siku zijazo.

 Akionyesha kuwa mkakati wa kiamisri haukupuuza hali ya Misri na jukumu la michezo na wanariadha kwa kuongeza nafasi ya mifano ya michezo na kufanya kazi kueneza maadili ya michezo kati ya vijana, pamoja na kutoa programu zilizolengwa zinazochangia uwekezaji mzuri wa wakati kati ya vijana, na maendeleo ya mifumo uwekezaji.  Iinaweka vifaa vya vijana na michezo ambavyo vijana wanatoa nguvu zao kwa njia ambayo inafaidi jamii, na tunafanya bidi zetu ili kufungua njia ya kufunua uwezo wa vijana katika shughuli za kiufundi, kisayansi na kitamaduni, na pia kuwapa mafunzo juu ya mazungumzo na kukubali wengine.  Juu ya kitambulisho cha kitaifa na urithi wetu wenye Heshima wa kitamaduni na wa kihistoria.

 Mkutano huo unajumuisha vikao vinane vya majadiliano kuzungumzia kundi la mihimili mikuu lililowakilishwa katika "jukumu la taasisi za kidini katika kupambana na ugaidi na msimamo mkali, familia, elimu na vyombo vya habari kama msingi wa kutega Msimamo mkali , Teknolojia kati ya kuhudumia na kukabiliana na ugaidi, ugaidi na vijana na vifaa vya kuendeleza uwezo wa kiteknolojia katika kupamba msimamo mkali na ugaidi ,"  Jukumu la nguvu laini katika kukabiliana na ugaidi na msimamo mkali, jukumu la taasisi zaJamii ya kiraia katika kukabiliana na ugaidi na msimamo mkali, "pamoja na  kuonyesha harakati maarufu za vijana zinazoshiriki katika matukio za mkutano huo.

 Kundi la vijana wa Kiarabu kutoka "Yemen, Yordani, Libya, Algeria, Palestina, Saudi Arabia, Bahrain, Kuwait, Iraqi, Morocco, Tunisia, Sudan na Comoros" nchi zinashiriki katika mkutano huo, pamoja na ushiriki wa ujumbe wa vijana wamisri.

Comments