"Sobhy " huandamana na Mawaziri wa vijana na michezo wa kiarabu katika ziara ya ukaguzi kwenye Kituo cha Olimpiki.
- 2020-01-06 12:19:54
Dokta Ashraf Sobhy , Waziri wa Vijana na Michezo, Mkuu wa Ofisi ya kiutendaji wa Baraza la Mawaziri waarabu kwa Vijana na michezo, alifanya ziara ya ukaguzi wa Kituo cha Olimpiki huko Maadi, akifuatana na vijana wa Kiarabu na mawaziri wa michezo walioshiriki katika shughuli za Mkutano wa mipango ya Vijana, kwa kutumia Teknolojia ya taarifa na uhusiano wake kuondokana na ugaidi, ambao shughuli zake zilianza asubuhi ya leo iliyoandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo katika jumuia ya Arabuni.
Mawaziri hao walitembelea sehemu za Kituo cha Olimpiki huko Maadi kuanzia hoteli ya makazi, uwanja wa mpira wa kisheria, viwanja vya pande tano, na kumbi zilizofunikwa za mafunzo ambazo ni pamoja na kumbi kadhaa za mafunzo kwa michezo mbali mbali, na mradi wa kuanzisha bwawa la kuogelea ndani ya kituo hicho.
Dokta Ashraf Sobhy alikagua uwezo wote wa kituo hiki na huduma inazopewa wachezaji wa timu za kitaifa, mwenyeji wa makambi yao ya mafunzo, na mipango yao ya kufikia mnamo mwaka mzima.
Waziri pia aligusia kushiriki mkutano wa mikutano ya mazungumzo ya vijana na mikutano ndani ya Kituo cha Olimpiki kwa kuzingatia miradi na mipango ya kutekelezwa na Wizara ya Vijana na Michezo kwa vijana wa Misri katika mikoa yote.
Kwa upande wao, vijana wa Kiarabu na mawaziri wa michezo na wajumbe waliofuatana walisifu muundo wa kipekee wa ujenzi katika Kituo cha Olimpiki huko Maadi, ambayo inafanya kuwa moja ya vifaa vikubwa na bora vya michezo Mashariki ya Kati, wakisifu huduma zinazotolewa na kituo hicho kwa timu zote za michezo na timu za kitaifa kwa mafunzo kwa kufuata mbinu za kisasa za kimataifa za michezo.
Comments