Matukio ya kikao cha tano cha mkutano wa mipango ya vijana chini ya anwani ya ( Jukumu la taasisi za jamii ya kiraia katika kupambana na ugaidi na ukali )

Matukio ya kikao cha tano cha mkutano wa mipango ya vijana chini ya anwani ya ( Jukumu la taasisi za jamii ya kiraia katika kupambana na ugaidi na ukali ) unaofanyika huko Jumuia ya mataifa ya kiarabu mnamo tarehe 4 hadi 6 Januari 2020, yamemalizikwa.


Mkutano unalenga kwa kueleza umuhimu wa jukumu la jamii ya kiraia katika kusimama kama msaidizi kwa nchi kwa ajili ya kupambana na ugaidi na ukali, pamoja na kuwahimiza vijana kwa ushiriki katika maisha ya kisiasa na kijamii, pia kuimarisha dhana ya kazi ya kujitolea unaolenga kwa kuunganisha vijana katika jamii na kuhifadhi  umoja wa jamii na mshikamano wake. 


Mkutano pia umejadili mawazo makali ya kiutamaduni yanayosimama kama kikwazo mbele ya maendeleo ya mataifa kwa sababu ya mawazo yake makale na yenye tofauti kulingana na mawazo ya kisasa na yanayozingatia kama kikwazo mbele ya jamii katika kukuza na kuendelea.


Kikao kimeongezwa na Dokta Noha Bakr ambaye ni mwanachama wa shirika la mashauri katika baraza la Kimisri kwa mawazo na masomo ya kimikakati, pia  profesa msaidizi  katika kitivo cha sayansi za kisiasa, chuo kikuu cha Marekani mjini Kairo, mwanachama katika kamati ya sayansi za kisiasa katika baraza la juu la utamaduni na Mwanachama wa baraza la Kimisri kwa masuala ya nje, kwa mahudhurio ya Dokta Samir Morkos ambaye ni mtafakariji wa kisiasa na mwandishi wa habari katika gazeti la Alahram, Dokta Ahmed Zayed ambaye ni profesa wa Sosholojia ya kisiasa na mkuu wa zamani wa kitivo cha Sanaa, chuo kikuu cha Kairo na mwanachama wa baraza la waamini wa chuo cha kitaifa kwa mafunzo, Bwana Hafez Abo Saada ambaye ni mkuu wa shirika la Kimisri kwa haki za binadamu na mwanachama wa baraza la kitaifa kwa haki za kibinadamu.

Comments