Donia Youssef, mchezaji wa timu ya kitaifa ya Misri ya Karate, alitwaa medali ya dhahabu ya Kiafrika kwenye mashindano ya Kata

 Donia Youssef Muhamad, mchezaji wa klabu ya Haras El Hedod na timu ya kitaifa ya Misri chini ya "miaka 18" kwa Karate, alishinda medali ya dhahabu katika Mashindano ya Afrika ya Watu wazima na Vijana "Wanaume na Wanawake" ambayo hufanyika  sasa hukoTunisia.


  Na Bingwa wa Misri na Haras El Hedod alipata  medali ya dhahabu katika shindano la "Kata" kulikuja baada ya kutoa utendaji mzuri wa kiufundi, ambapo alishinda medali ya dhahabu bila ya ushindani.


 Donia alichaguliwa kujiunga na safu ya timu ya Misri , baada ya kupata nafasi ya kwanza katika mkoa wa Aleskandaria, kwenye mashindano ya "kata" ya

wasichana na wanawake .


 Donia Ana  ukanda mweusi "1 Dani" na anachezea Klabu ya Haras El Hedod inayosimamiwa na Kocha Magdy Ali Abdel Hamid, anayeongoza mfumo wa karate kwa klabu ya Haras El Hedod, na sasa  klabu ile inashiriki katika hatua 8 kwenye Ligi Kuu ya Karate na wachezaji 52 .  Kocha  Magdy ana matumaini ya kuwakilisha bingwa wa Olimpiki, Kama mmoja wa mabingwa wa Haras El Hedod.

Comments