Kamerun Ni timu ya kitaifa bora zaidi kwa mpira wa miguu ya wanawke barani Afrika mwaka 2019

Kamerun ilipewa tuzo ya timu ya mpira wa miguu ya wanawake  bora zaidi barani Afrika mwaka 2019 , Kulingana na Shirikisho la Kiafrika  la mpira wa miguu (CAF).


Na sherehe ya tuzo bora  zaidi barani Afrika 2019, ilifanyikwa jana , siku ya Jumanne huko Hurghada.


Kamerun, Nigeria na Afrika Kusini zilishindania tuzo hiyo.


Timu hizo tatu zilishiriki katika Kombe la Dunia lililopita  wakati wa majira ya joto huko Ufaransa.


 Afrika Kusini ilicheza Kombe la Dunia la kwanza kwake, lakini ilitoka kutoka mashindano hayo bila alama, wakati  ambapo Kamerun na Nigeria zilifikia raundi ya pili.

 

Wanawake wa Kamerun watacheza pamoja na  Zambia mwezi huu  ili kupata kadi ya kufikia Olimpiki ya Tokyo 2020.

Comments