Mwaalgeria Gamal Bel Madi kocha wa timu ya kitaifa ya Algeria alishinda tuzo ya kocha bora zaidi barani Afrika 2019 kulingana na yaliyotangazwa kwa Shirikisho la Kiafrika la mpira wa miguu (CAF) . Na jioni ya siku ya Jumanne sherehe ya tuzo za bora zaidi barani Afrika 2019 ilifanyika mjini mwa Hurgada nchini Misri .
Na watatu waliogombea tuzo ni : kutoka Senegal Alio Siseh kocha wa Senegal , kutoka Algeria Gamal Bel Madi kocha wa Algeria na kutoka Tunisia Moeen Shaabani kocha wa Tunisia
Na Gamal Bel Madi aliongoza timu ya Algeria ili kushinda mashindano ya kombe la mataifa ya kiafrika yaliyofanyika wakati wa Majira ya joto yaliyopita nchini Misri ambapo Algeria ilishinda taji yake ya pili baada ya kutokuwepo kwake kwa muda mrefu tangu ushindi wake wa kwanza nchini Algeria 1990.Na Alio Siseh alifanikiwa kufikisha nchi zake fainali ya kombe la mataifa ya kiafrika kwa mara ya pili katika historia yake isipokuwa Siseh alishindwa kombe pamoja na Senegal kama kocha hali kadhalika kushindwa kwake kama mchezaji 2002.
Ama Moeen El Shaabani aliendelea kushinda mashindano kwa ligi ya mabingwa Afrika kwa msimu wa pili mfululizo
Comments