"Waziri wa Michezo anahudhuria sherehe ya Siku ya Michezo ya Kiafrika katika Kituo cha Olimpiki huko Maadi"

Waziri wa Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhy alishuhudia Siku ya Michezo ya Kiafrika iliyoandaliwa na Ubalozi wa kamerun huko Kairo,  na kwa kuwepo kwa Mabalozi wa Burundi, Côte d'Ivoire, Uganda na Mali.

 

 Waziri wa Vijana na Michezo aliwapongeza Balozi wa kamerun, na wanachama wa jamii za Kiafrika, akisisitiza uhusiano wa kina kati ya Misri na nchi za Afrika chini ya urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika, na anatamani kwao maendeleo zaidi ,mafanikio na ustawi.

 

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mabalozi wa kiafrika Balozi Mohamed Labranj Balozi wa Jamhuri ya kamerun nchini Misri akisisitiza kwamba Uandaji wa Kombe la Mataifa ya kiafrika huko Misri Ni jambo muhimu zaidi kwa serikali ya Misri inayoongozwa na Rais Abdel Fattah al-Sisi, na Ushindi wa Misri au kamerun ni ushindi mmoja nasi, Misri ni nchi kubwa na mama wa Afrika. Kukaribisha Misri kwa michuano hiyo ni fahari kwa bara zima kwa sababu ya historia yake kubwa katika kimichezo na kiuchumi

 

Mkuu wa mabalozi wa kiafrika alishukuru Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo wa kimisri kwa kuhudhuria kwake mwisho wa matukio Na kuwepo kwake wa kudumu na ushiriki  wake katika sherehe zote za kiafrika zinazooandaliwa huko nchini Misri.

Comments