Yassmin Hamdy anashinda medali ya shaba ya michuano kwa Karate ( Series A ) nchini Chile

Yassmin Hamdy Atia, mchezaji wa timu ya kitaifa ya Misri kwa Karate  ameshinda medali ya shaba katika mashindano ya uzito wa kilogramu 55 katika michuano ya ( Series A) inayofanyika mnamo kipindi cha tarehe 10 hadi 12 Januari nchini Chile, na hii ni michuano ya kwanza ya uainishaji wa Olimpiki kwa mwaka huu.


Yasmin ameshinda medali ya shaba baada ya ushindi wake mbele ya mchezaji wa Italia ( Lorena Bosa) kwa  0-5 katika mechi ya kuainisha mshindi kwa medali ya shaba.


Yassmin amehakikisha njia nzuri katika michuano hiyo, ambapo ameshinda katika mechi yake ya kwanza dhidi ya mchezaji wa Norway kwa  0-5, kisha akashinda mbele  ya mchezaji wa Ujerumani kwa  0-4, pia akashinda mbele ya mchezaji wa Morocvo kwa  3-7, hii kabla ya kushindwa kwake mbele ya mchezaji wa Ukraine kwa  3-0 katika mechi yake ya mwisho katika duru ya kwanza.

Misri inashiriki katika mashindano ya michuano hiyo kwa wachezaji wanane ( wanawake 5 na wanaume 3).


Timu inaongozwa na wakurugenzi wa kiufundi ( Mohamed Abd Alrahman) na (Mohamed Abd Alregal), na ujumbe unaongozwa na ( Dokta Walid Alhelaly).


Michuano inafanyika mjini Santiago, nchini Chile kwa ushiriki wa wachezaji 466 wanaowakilisha nchi 65.


Michuano hiyo inazingatiwa michuano ya kwanza mnamo mwaka huu katika kuendelea kwa njia ya kufikia Olimpiki, mabingwa wa karate wanahangaika kuboresha safu yao ya Olimpiki itakayofikia Olimpiki za Tokyo 2020.


Comments