Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alitoa uamuzi wa kuanzisha Jumuiya ya kutoa Huduma bura ya Umma kwa Vijana kulingana na vifungu vya Ibara ya 23 ya Sheria ya Kuandaa Taasisi za Vijana, na makao makuu yake yatapatikana katika Diwani ya Wizara hiyo, na inasimamiwa na Idara Kuu kwa Mipango ya kiutamaduni na kijitolea kwenye Wizara hiyo katika masuala yote ya kiufundi, kifedha na kiutawala na kutekeleza majukumu yaliyowekwa kwa hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazopanga Shirika.
na uamuzi wa waziri uliambatana na kutoa kanuni zake, ambapo sehemu ya kwanza ya orodha hiyo ilikuwa chini ya kichwa cha "Maelezo - Vifungu Vikuu" kwa ajili ya kufafanua majukumu kwa ujumla kwa shirikisho, yanayofupishwa kwa ufadhili wa utumiaji bure wa umma kwa vijana, ambapo litahusika na mambo yake kwa uaminifu, na linafanya uwezo wake katika mfumo wa sera kuu ya serikali na mipango iliyowekwa na mamlaka. , na kuweka sera ya jumla ya harakati ya kutoa Huduma bure za umma kwa vijana.
Imetajwa katika sheria kuwa majukumu ya Shirikisho ni pamoja na kufanya kazi ni kueneza roho ya kujitolea ya umma, kuandaa ushiriki katika mikutano ya hadhara ya kikanda, kitaifa na kimataifa ya kujitolea na mikutano kwa vijana, na kufanya kazi kutekeleza miradi ya umma katika uwanja wa huduma ya kujitolea inayohusiana na mpango wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi , pamoja na kuchangia kuandaa maadhimisho na hafla, linalotakiwa kufanyika na Waziri wa Vijana na Michezo (waziri Mhusika).
Na sehemu ya pili ya orodha hiyo ilikuja kufafanua vifungu vya Uanachama katika Shirikisho hilo kulingana na aina ya Uanachama wa vijana waliojitolea kwenye Shirikisho na taratibu na masharti ya Uanachama , na usimamizi wa Shirikisho umeazimia kutosheleza rekodi maalum ya usajili wa uanachama inayojumuisha jina na data ya mwanachama, na tarehe ya uamuzi wa bodi kukubali Uanachama wake, na maombi ya Uanachama yamewasilishwa kwa utawala wa Shirikisho hilo Kwenye fomu husika kwa hiyo, Bodi ya Wakurugenzi ya Shirikisho itaamua katika yanayohusu maombi yote ya uanachama.
Sura ya tatu ya orodha ilionyesha majukumu ya bodi ya wakurugenzi, mkutano mkuu, na usimamizi wa masuala ya Shirikisho kupitia bodi ya wakurugenzi inayotoa uamuzi wa kumteua kutoka Waziri wa Vijana na Michezo, ilimradi baraza hilo lina (wanachama 3 zaidi ya umri - wanachama 5 wachanga, miongoni mwao mwanamke mmoja - wakilishi 2 kwa Wizara ya Vijana na Michezo) na wakati wa mkutano wao wa kwanza watachagua miongoni mwao mkuu mmoja , na muda wa baraza utakuwa miaka 4 tangu tarehe ya kuteuliwa kwake.
Sura ya tatu pia ilielezea madaraka yote ya Bodi ya Wakurugenzi na masharti yanayopaswa kutekelezwa na wajumbe kwa kuwa mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ni wa utaifa wa Misri anayepata haki kamili ya Uraia, angalau kuwa na cheti cha juu , na asiyekuwa na hukumu za mwisho zilizotolewa dhidi yake na adhabu ya jinai au makosa. aliyemalizika jeshi yake ya lazima au kuachiliwa kutoka kwa hiyo, au kutohitajika kuifanya kwa mujibu wa kaida za kisheria, na kuwa na mwenendo na sifa nzuri .
Imepangwa kuwa Wizara ya Vijana na Michezo itangaze, mnamo kipindi kijacho, maelezo yote yanayohusiana na kujiunga na Shirikisho na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ili kuanza majukumu yake yanayohitajika kwa haraka iwezekanavyo .
Comments