Kama naibu wa Waziri wa vijana na michezo.... El-kordy anaheshimu timu ya kitaifa ya Misri kwa Karate
- 2020-01-16 20:29:53
Jioni ya leo, Mohamed El-kordy ambaye ni msaidizi wa waziri wa vijana na michezo wa masuala ya michuano na kama naibu Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa vijana na michezo anawaheshimu wachezaji wa timu ya kitaifa za karate za wavulana, vijana na chini ya miaka 23 walioshinda medali mbalimbali katika michuano ya dunia iliyofanyika nchini Chile, pamoja na timu ya kitaifa ya wanaume ambayo imeshiriki katika michuano ya tuzo kuu nchini Uhispania.
Balozi wa Japan , Balozi wa Chile na Fathy Nada ambaye ni Mkuu wa shughuli za kimichezo pamoja na baraza la uongozi, idadi ya wenyekiti wa klabu na mashirikisho ya kimichezo mengine walihudhuria sherehe hiyo.
El-kordy amesisitiza kuwa heshimu imekuja miongoni mwa mbinu za Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa vijana na michezo katika kuwaheshimu wachezaji, na miongoni mwa siasa ya nchi ili kuunga mkono na kuwaheshimu wachezaji bora wa riadha katika michezo mbalimbali, pamoja na kuwahimiza wachezaji wengine kwa ajili ya kufanya juhudi zaidi ili kuhakikisha tija zisizo za kawaida katika mashindano yanayofuata.
Akiongeza kwamba wizara inajali daima kwa kuongeza kiwango cha wachezaji wanaowakilisha Misri katika michezo mbalimbali kupitia kufanya makambi mbalimbali na zinazoshiriki katika michuano, hii kwa ajili ya kuwaandaa kwa mashindano muhimu katika kipindi kijacho ambayo mashindano muhimu zaidi ni kikao cha michezo ya Olimpiki, itakayofanyika mjini Tokyo mnamo mwaka huu.
Imetajwa kuwa Misri imechukua nafasi ya kwanza baina ya nchi zilizoshiriki katika michuano ya dunia nchini Chile kwa medali 19 mbalimbali.
Katika muktadha huo huo, timu ya kitaifa ya kwanza itaheshimika baada ya ushiriki wake katika michuano ya tuzo kuu nchini Uhispania, ambapo Yasmin Hamdy amehakikisha medali ya kidhahabu na Radwa Sayed ameshinda medali ya shaba.
Comments