El-shobokshy ni Mmisri wa kwanza anayeshinda medali ya shaba ya kikao cha michezo ya msimu wa baridi kwa urambazaji wa kuteleza juu ya barafu
- 2020-01-19 11:39:09
Mchezaji Mmisri ( Khaled El-shobokshy) ameshinda medali ya shaba katika kikao cha michezo cha kimataifa cha msimu wa baridi kwa urambazaji wa riadha wa kuteleza juu ya barafu kilichofanyika nchini Austria, na amepata nafasi ya tatu ya michuano ya dunia kwa kuteleza juu ya barafu, na hii ni medali ya kwanza ya aina yake katika michezo hiyo kwa mchezaji Mmisri, Mwarabu na Mwafrika, pia ameheshimiwa na kamati iliyoandaa michuano ya dunia ya kuteleza juu ya barafu.
Meja Jenerali Dokta ( Moanes Abo Aouf ) mwenyekiti wa shirikisho la Kimisri kwa urambazaji wa riadha, amesisitiza kuwa medali hiyo ni ya kwanza ya aina yake katika michezo ile, na tumeweza kuhakikisha mafanikio katika michezo hiyo kwa mawazo mapya na ya kipekee, pamoja na kukidhi uwanja wa barafu katika eneo fulani la sekta kibinafsi, na tulileta Kocha Mfaransa kwa muda wa siku 18 kama kujitolea na hakupata yoyote, pia kukidhi tekiti za ndege kwenda na kurudi kutoka shirika la ndege bila ya yoyote ya fedha, na vyombo vyote vya wachezaji wanaovihitajika katika mazoezi kutoka kampuni fulani kibinafsi ili kuwakidhi wachezaji njia zote za mazoezi na mafanikio bila ya gharama za kifedha zozote juu ya shirikisho au hata nchi, kwa mujibu wa maagizo ya Waziri wa vijana na michezo Dokta Ashraf Sobhy anayejali michezo hii kwa kiwango kikubwa tangu nilipochukua uongozi wa shirikisho miezi sita iliyopita, na Dokta Moanes Abo Aouf amemaliza maneno yake kwa kusema kwamba kuna mpango ili kuimarisha michezo ya urambazaji wa riadha mnamo kipindi kijacho.
Comments