Misri inaishinda kenya katika mechi ya pili ya mataifa ya Afrika kwa mpira wa mikono

Timu ya kitaifa ya Misri  ya mpira wa mikono kwa uongozi wa kocha mhispania wa kiufundi Roberto barando ilishinda mwenzake wa kenya kwa  44-19 katika mzunguko wa pili wa kiwango cha kwanza katika mashindano ya mataifa ya kiafrika ya mpira wa mikono yanayofanyika kutoka 16 hadi 26 mwezi wa Januari  nchini Tunisia yanayofikisha Olimpiki ya Tokyo 2020 na kombe la dunia 2021 


Na mafarao wanadhibiti mechi mwanzoni mwake ambapo walimaliza nusu ya kwanza ya mechi  kwa  21-7


Na orodha ya mafarao imejumuisha wachezaji 16 katika mechi ya kenya nao ni:


Golikipa : Karim Hindawi - Issam Al-Tayyar. 

Mrengo wa kulia: Muhammad Sanad - Yahya Khaled. 

Upande wa kulia: Ahmed Al-Ahmar - Mohsen Ramadan

 Wafungaji: Ahmed Hisham - Saif Al-Daraa. Upande wa kushoto: Yahya Al-Daraa - Ali Zain - Hassan Qaddah. 

Mrengo wa kushoto: Omar al-Wakeel - Ahmed Moamen. 

Mchezaji wa duru: Wissam Nawwar - Khaled Walid - Muhammad Mamdouh


Na mchezaji wa timu ya kitaifa ya Misri  Mohsen Ramadan alipata tuzo ya mchezaji Bora kabisa mechini 


Na inaamuliwa kwamba mafarao watapumzika kesho kabla ya kumalizia mechi ya kiwango cha kwanza siku ya jumapili 19 mwezi wa januari kwa kukabiliana kwa Congo ya kidemokrasia mnamo saa moja jioni. 


Na Misri  iko katika kikundi cha kwanza pamoja na timu za kitaifa za Geunia , Kongo  ya kidemokrasia na Kenya  na kikundi cha pili kinajumuisha timu za kitaifa za Angola , Gabon , Libia na Nigeria wakati ambapo Tunisia iko katika kikundi cha tatu pamoja na timu za kitaifa za cameron , Cote d'Ivoire na Cape Verde na kikundi cha nne kinajumuisha Algeria , Morocco , Kongo  na Zambia

Comments