"Chuo cha kitaifa kwa Mafunzo " kinakaribisha wanawake 95 wanaoshiriki katika Programu ya Uongozi kwa Wanawake wa Kiafrika
- 2020-01-20 12:00:10
Dokta Rasha Ragheb, Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha kitaifa kwa Mafunzo , aliupokea ujumbe wa kutembelea kutoka Taasisi ya Usimamizi ya Kitaifa inayojumuisha wanawake 95 wa Kiafrika wanaoshiriki katika mpango wa uongozi wa kiutendaji kwa wanawake wa Kiafrika, ili kuimarisha mawasiliano kati ya pande hizo mbili na kutambulisha programu za Chuo, hasa zile zinazohusika na masuala ya vijana na suala la Kiafrika, kama vile Programu ya Urais kwa kuwawezesha Vijana wa Kiafrika kwa Uongozi APLP . na Programu ya kuwawezesha watendaji waafrika kwa Uongozi LEP.
Rasha Ragheb akaribisha ujumbe uliotembelea kutoka Taasisi
ya Kitaifa inayojumuisha Dokta Rehab Farraj, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo
na Uwezo wa Binadamu, Dokta Hanan Rizk, Mshauri kwa Mkurugenzi Mtendaji, Bibi
Mai Al-Shami, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, na Dokta Dina,
Mkurugenzi wa Idara ya sekta ya Ajira , na wanawake waafrika.
Rasha Ragheb alielezea furaha yake na ujio wa wageni wa
kiafrika kuelekea Misri na Chuo cha kitaifa, na
kwa haraka alizungumzia jukumu la
taaluma na programu ambazo hutoa kama programu za Urais, pamoja na Programu ya
Urais ya kuwawezesha Vijana waafrika kwa Uongozi ulioanza mnamo Agosti 2019, na
kile wanachokipata kutoka kama mada zenye faida kubwa sana, na mifumo ya kuiga kama mfumo wa kuiga Umoja
wa Afrika AU, usimamizi wa shida, na kadhalika , vile vile Programu ya Urais
kwa kuwawezesha vijana kwa Uongozi, na Programu ya Urais kwa kuwawezesha
watendaji kwa Uongozi inayolenga kikundi cha umri wa miaka 30 hadi 45, na
akasema kwamba Chuo hicho kinakusudia mnamo
mwaka 2020 kuwafundisha wanafunzi 11800.
Sarah Yakout, Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo hicho,
alitoa maonyesho ya utangulizi juu ya Chuo cha Mafunzo ya Kitaifa na wazo la
kuanzishwa kwake, na kwamba Chuo hicho kila wakati kinatafuta kufikia maadili
ya uadilifu, uwazi, ushirikiano na kuheshimiana, na pia alizungumzia mipango
inayotolewa kwa Chuo hicho, ambacho hadi sasa kilifikia programu 57 za mafunzo,
ambapo Chuo hicho kinapeana aina tatu za programu, ambazo ni. Mipango
iliyowasilishwa kwa mashirika ya utendaji, mipango ya Urais, na mipango ya
kimataifa.
Aliongeza kuwa Programu ya kuwawezesha watendaji waafrika
kwa Uongozi inawalenga wafanyikazi 200 kutoka nchi 27 za Kiafrika kwa ajili ya
kuwanufaisha kwa maarifa na ujuzi ambao
utawawezesha kushinda Ufisadi na urasimu, na kwamba Programu ya Urais kwa
kuwawezesha vijana kwa Uongozi ni pamoja na vijana wenye umri wa miaka 18 hadi
30 wanaowakilisha nchi 50 za Kiafrika katika viunga vitatu.
Programu ya Uongozi wa kiutendaji kwa Wanawake waafrika
inayotolewa kwa Taasisi ya Usimamizi wa Kitaifa inakusudia kuongeza maarifa na
ujuzi wa wanawake wa Kiafrika ambao tayari wameshafikia nafasi za umuhimu
katika serikali za Kiafrika ili kuongeza ufanisi wao na athari, na hutoa jukwaa
la maingiliano la mafundisho kwa wanawake wa Kiafrika ambao ni wanawake 95
wanaowakilisha nchi 40 za kiafrika, na inalenga Programu zote zinazotolewa kwa
Waafrika, iwe ni kutoka Chuo cha kitaifa cha Mafunzo au Taasisi ya Kitaifa ya
Ukamilifu na Ushirikiano wa kiafrika kama sehemu ya Mkakati wa Afrika 2063.
inayopaswa kutaja kuwa wazo la Mpango wa Urais kwa kuwawezesha
Vijana waafrika kwa Uongozi lilizinduliwa na Rais Abd El Fatah El-Sisi kutoka
Sharm El-Sheikh, kama moja ya mapendekezo ya Mkutano wa Vijana wa
Ulimwengu mnamo Novemba 2018, na Chuo
cha Mafunzo cha Kitaifa kilianza kutekeleza sawa sawa na urais wa Misri kwa
Umoja wa Afrika kwa mwaka wa 2019, wakati ambapo Misri ni sehemu muhimu ya bara
Afrika hufungamana kwa vifungo vya Ndugu. Programu hiyo inakusudia kuleta
pamoja vijana wa Kiafrika kutoka nchi zote za bara katika mpango mmoja wa
mafunzo na ushirika na imani tofauti chini ya mwavuli mmoja unaolenga Maendeleo
na Amani. Chuo hicho pia kinatoa mpango wa kuwawezesha watendaji waafrika kwa
Uongozi LEP tangu Septemba 2019, ambayo
hadi sasa imewapa mafunzo wafanyikazi wa serikali 107 kutoka nchi 27 za kiafrika
Comments