Misri inakaribisha Mashindano ya Upigaji upinde ya Kiarabu na Mashindano ya Sheikha Fatima binti Mubarak kwa upigaji upinde wa wanawake mnamo mwezi wa Februari
- 2020-01-22 11:19:31
Shirikisho la upigaji upinde la kimisri, lililoongozwa na Meja Jenerali Hazem Hosni, lilitangaza kuwa Misri itakaribisha shughuli za Mashindano ya 15 ya Kihistoria ya upigaji upinde kwenye sahani za hewa, na mashindano ya Sheikha Fatima binti Mubarak ya upigaji upinde la Kimataifa kwa Wanawake, yatakayoanza shughuli zake kutoka tarehe 17 hadi 26 Februari, na yatafanyika kwenye viwanja vya Klabu ya upigaji upinde katika eneo la elharam na Klabu ya El Seed katika eneo la 6 Oktoba
wapigaji upinde 350 kutoka wanawake na wanaume kutoka nchi 13 watashiriki katika mashindano hayo, nazo ni "Tunisia, Morocco, Algeria, Syria, Yemen, Kuwait, Lebanon, Emirates, Kuwait, Bahrain, Iraq, Sultanate ya Oman, na Misri" kama nchi mwenyeji.
Inatarajiwa kwamba hafla ya ufunguzi itafanyika mnamo februari 18 katika moja ya hoteli kuu huko Kairo. Sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo zitashuhudia watu kadhaa mashuhuri nchini Misri na ulimwengu wa Kiarabu.
Hii inakuja katika mfumo wa kuunga mkono Wizara ya Vijana na Michezo inayoongozwa na Dokta Ashraf Sobhy, ambaye hutoa kipaumbele kwa hafla na matukio yote yaliyoshikiliwa na Wamisri katika mashindano mbali mbali ya Shirikisho la upigaji upinde la kimisri.
Katika suala hili, Meja Jenerali Hazem Hosni alisisitiza kwamba mwenyeji wa Mashindano ya Kiarabu ni mwendelezo wa mfululizo wa mashindano yaliyoshikiliwa na Wamisri katika upigaji upinde , na hutoa msukumo mkali kwa wapigaji upinde wamisri kupitia ushindani na mabingwa wa Kiarabu ili kuwastahili kushiriki katika ubingwa wa dunia na mashindano ya Olimpiki ijayo. akimshukuru dokta Ashraf sobhy waziri wa vijana na michezo kwa Kutoa msaada wa kila aina kwa shirikisho
Hosni aliashiria kwamba michuano ya kiarabu inashikilia ushindani mkali kila mwaka kutokana na kiwango cha pekee ambacho nchi za Kiarabu zimekifikia kwa upigaji upinde , haswa nchi za Ghuba zilizoendeleza sana katika silaha na sasa zina mabingwa wa kiwango cha dunia.
Rais wa Shirikisho la Upigaji upinde alisema kwamba mabingwa hawa huunga mkono sana utalii wa michezo nchini Misri, na anathibitisha uwezo wa Misri kukaribisha hafla kubwa na ujumbe kwa wote kwamba Misri ni nchi ya usalama na inakaribisha ndugu na jamaa wote.
Comments