Waziri wa Vijana na Michezo anashuhudia mkutano wa waandishi wa habari ili kutangaza uzinduzi wa mbio ya "Nusu ya mashindano ya piramidi "

Jumatano Dokta Ashraf Sobhy  Waziri wa Vijana na Michezo, alishuhudia shughuli za mkutano wa waandishi wa habari kutangaza maelezo ya mbio ya "Nusu  mashindano ya Piramidi ", ambayo hufanyika chini ya uangalizi wa Wizara ya Vijana na Michezo,  Wizara ya Utalii na wizara ya  Vitu vya kale.



Mkutano huo wa waandishi wa habari ulihudhuriwa na Dokta Seif Allah Shaheen  Rais wa Shirikisho la michezo ya Misri, Ayman Hakki  Mwanzishi na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya (TriFactory), viongozi kadhaa wa Wizara ya Vijana na Michezo, na kundi la wataalamu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari.



Katika hotuba yake, Waziri wa Vijana na Michezo alisema: "Shughuli hii inakuja ndani ya mkakati wa wizara ya kupanua  kwa msingi wa mchezo wa Mbio na kujali afya, na tuna hamu kubwa ya kufanyika kukimbia iwe njia ya maisha kwa Wamisri wote, na daima tunafurahi  kushirikiana kuandaa shughuli kama hizi,  zinazochangia kwa kiasi kikubwa kukuza kuwepo kwa nchi yetu mpendws Misri kwenye ramani ya utalii wa kimichezo. "



Kwa upande wake, Ayman Haki  Mwanzishi na Mwenyekiti wa Kampuni ya (TriFactory), alisema "ninamshukuru Waziri wa Vijana na Michezo kwa kudhamini shughuli hii na ushirikiano kupitia Wizara ya Vijana na Michezo (Idara kuu ya Utalii wa kimichezo), na mashindano hayo hufanyika kwa mwaka wa pili mfululizo, na wanapewa nafasi ya kushiriki katika umbali wa tatu unaopatikana  yoyote ambayo ni km 21 na 10 km, pamoja na 6 km".



Haki alisema: "Baada ya kufanikiwa kwa toleo la kwanza mwaka jana, mbio za"nusu  mashindano ya Piramidi  "mwaka huu zitajumuisha njia mpya kwa ushiriki wa wanariadha kutoka kote ulimwenguni kwenye eneo la piramidi. Mbio za mwaka jana zilihudhuriwa na washindani 3,600 waliowakilisha nchi 77, na tuna hamu kubwa katika viwango vya kimataifa. Hii inatufanya tuweze kuvutia wataalamu na kushiriki kwenye mbio. 

Comments