Misri inashinda Angola katika robo fainali ya kombe la mataifa ya Kiafrika kwa mpira wa mikono

Timu ya kitaifa ya kwanza ya wanaume ya mpira wa mikono chini ya mkurugenzi wa kiufundi Mhispania (Roberto Garissa), amehakikisha ushindi dhidi ya timu ya kitaifa ya Angola kwa  (33-26) katika mechi iliyofanyika kati yao miongoni mwa mechi za awamu ya pili ya zamu ya robo ya fainali, katika michuano ya kombe la mataifa ya Kiafrika inayofanyika sasa nchini Tunisia na itaendelea mpaka siku ya 26 ya mwezi huu wa Januari.


Timu ya kitaifa ilikuwa imehakikisha ushindi katika awamu ya kwanza dhidi ya timu ya kitaifa ya Gabon kwa  (36-17).


Timu ya kitaifa sasa hivi inachukua nafasi ya kwanza katika kundi lake kwa pointi 6, ili kufikia zamu ya nusu ya fainali, na timu ya kitaifa ya Angola inakuja katika nafasi ya pili kwa pointi 4.


Orodha ya timu ya kitaifa inajumuisha wachezaji 21 nao ni : Karim Hendawy, Mohamed Esam Altayar, Mohamed Aly, Ibrahim Almasry, Mohamed Mamdouh Hashem, Wesam Samy, Khaled Walid, Ahmed Adel, Mohamed Sanad, Akram Youssry, Ahmed Alahmar, Yehia Khaled, Mohsen Ramadan, Ahmed Khairy, Seif Alderaa, Ahmed Hesham, Yehia Alderaa, Aly Zein, Hassan Kadah, Omar Bakar na Ahmed Moamen.


Michuano hiyo kwa mara ya kwanza inashuhudia ushiriki wa timu ya kitaifa 16, zinashindana kwa lakabu ya michuano hiyo, ambapo timu ya kitaifa yenye nafasi ya kwanza tu itafikia Olimpiki za Tokyo 2020, huku timu za kitaifa zenye nafasi kutoka nafasi ya kwanza hadi nafasi ya saba zitapatia kadi ya kushiriki katika michuano ya dunia 2021 nchini Misri.

Comments