Udhamini wa "Nasser" kwa Uongozi wa kimageuzi hutiliwa umuhimu mkubwa sana toka nchi na Taasisi kuu kwa Maarifa inatoa mtandao wa kielektroniki kwa udhamini kwa lugha nane(8) tofauti.
- 2019-05-20 13:34:04
Wizara ya Vijana na Michezo, inayoongozwa na Dokta Ashraf Sobhy, inasisitiza umuhimu wa shime na usaidizi wa nchi kwa suala la kiafrika, kwa mujibu wa tangazo la Rais wa Jamhuri wakati wa matukio ya Kongamano la Vijana wa Ulimwengu, ambalo lilishuhudia uwakilishi wa heshima kwa vijana wa nchi za kiafrika, ambapo udhamini wa"Nasser kwa Uongozi wa kimageuzi" iliyoandaliwa na (Idara kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia - Ofisi ya Vijana wa kiafrika ) mnamo kipindi cha tarehe 8 hadi 22 Juni ijao; inayoelezea shime ya Serikali kwake na imani yake kwa jukumu la vijana wa Kiafrika na umuhimu wa kutoa aina zote za msaada, ,kuwaimarisha wataalamu na kuwapa mafunzo,na kuwawezesha katika nafasi za uongozi na kufaidika na uwezo na mawazo yao.
Katika muktadha huu Taasisi kuu kwa Maarifa kupitia lango la elektroniki lilizinduliwa sambamba na Uraisi wa Misri wa Umoja wa kiafrika, ambalo linakusanya Tovuti saba za mtandao wa inteneti kwa lugha zifuatazo:, Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa. Kiswahili , Kihausa ,Kiamhari, na Kireno http://africa.sis.gov.eg /
Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi" uliotolewa kwa Wizara ya Vijana na Michezo, chini ya uongozi wa Dokta Ashraf Sobhy, na hayo yanakuja katika utekelezaji wa mpango wa kuwawezesha vijana milioni moja wa kiafrika ifikapo mwaka wa 2021 ,ambayo ilizinduliwa na Kamisheni ya Sayansi Teknolojia na Rasilimali za watu wa Umoja wa kiafrika hivi karibuni Mjini Mkuu wa Ethiopia "Addis Ababa".
Mamlaka Kuu ya Maarifa pia ilichapisha Udhamini kwenye tovuti yake rasmi http://www.sis.gov.eg kwa lugha tatu: Kiarabu, Kiingereza na Kifaransa kupitia tovuti inayohusu udhamini huo ambayo unayajumuisha masharti ya kujiunga kwenye Udhamini na fomu ya usajili.
Inasemwa kwamba Wizara ya Vijana na Michezo ilitangaza kuwa Udhamini huo unawalenga Vijana 120 toka viongozi watendaji wa nchi wanachama za Umoja wa kiafrika, watoaji maamuzi katika sekta ya serikali, viongozi watendaji katika sekta binafsi, vijana wa jamii ya kiraia, wakuu wa mabaraza ya kitaifa kwa vijana, maprofessa wa vyuo vikuu, watafiti katika vituo vya tafiti za kimkakati na kimawazo, wanachama wa vyama vya kiufundi na waandishi wa habari.
Udhamini unalenga kuhamisha jaribio kubwa la kimisri la kujenga taasisi za kitaifa na kuunda kizazi kipya cha viongozi wa mabadiliko ya vijana wa kiafrika wenye Maoni yanayosawazisha na maelekezo ya Urais wa Misri wa Umoja wa kiafrika, yenye imani ya kuhudumia malengo ya Umoja wa kiafrika kupitia ushirikiano, pamoja na kuanzisha mkusanyiko wa viongozi vijana wa Afrika wenye nguvu zaidi barani, na kwa mafunzo, umahiri unaolazimika na maoni ya kimikakati.
Pia Udhamini wa"Nasser" unazingatiwa ni Udhamini wa kwanza wa (kiafrika_kiafrika) unaolenga viongozi vijana watekelezaji wa kiafrika wenye Nyanja tofauti za utekelezaji ndani ya jamii zao,Udhamini pia ni mojawapo ya vipengele vya uwezeshaji muhimu kwa mabadiliko ya kiafrika yaliyoidhinishwa kwa Ajenda ya Afrika 2063.
Comments